RAIS Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imeazimia kutoa kipaumbele na kusimamia kikamilifu upatikanaji wa ajira kwa vijana

RAIS  Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imeazimia kutoa kipaumbele na kusimamia kikamilifu upatikanaji wa ajira kwa vijana

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imeazimia kutoa kipaumbele na kusimamia kikamilifu upatikanaji wa ajira kwa vijana wa Kijiji cha Dundua  katika miradi mbali mbali itakayoanzishwa katika eneo lililotengwa la ujenzi wa Bandari ya Mafuta na Gesi Mangapwani. Alhaj Dk. Mwinyi ametoa ahadi hiyo  katika

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imeazimia kutoa kipaumbele na kusimamia kikamilifu upatikanaji wa ajira kwa vijana wa Kijiji cha Dundua  katika miradi mbali mbali itakayoanzishwa katika eneo lililotengwa la ujenzi wa Bandari ya Mafuta na Gesi Mangapwani.

Alhaj Dk. Mwinyi ametoa ahadi hiyo  katika hafla ya Ufunguzi wa Msikiti na Madrasa ya Nuru –al – Yaqin, uliopo kijiji cha Dundua Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema hatua ya wananchi wa Kijiji cha Dundua kukubali kuhama katika eneo lao la makaazi ya  asili na kupisha mradi mkubwa wa Ujenzi wa Bandari ya Mafuta, utakaohusisha Bandari kadhaa, ulikuwa ni wa kizalendo na ulioweka mbele maendeleo ya nchi.

Alisema Serikali itasimamia uendelezaji wa eneo hilo, ambapo sharti la kwanza kwa Mwekezaji yoyote itakuwa ni kuwapatia nafasi za kazi vijana wa Dundua.

Alisema mradi utakaotekelezwa katika eneo hilo ni mkubwa sana, hivyo akawataka vijana kuwa tayari kwa ajili ya kufanya kazi.

“Niwaambie wazazi mmefanya jambo jema na manufaa yake sio kwa  nchi tu bali hata kwa wananchi”, alisema.

Alhaj Dk. mwinyi alieleza kuwa eneo walilohama wananchi hao litaingizwa katika michoro kwa ajili ya miradi mikubwa ya Bandari ya Mafuta na kukabidhiwa serikalini.

Alieleza kuwa katika hatua ya kufanikisha mchakato wa kupisha eneo hilo la asili kwa   shughuli hizo za maendeleo hadi sasa wapo baadhi ya wananchi ambao hawajaridhika na hatua hiyo.

Rais Dk. Mwinyi aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, awamu ya saba kwa kubuni jambo hilo linalofaa kuigwa na kuendelezwa la kuhakikisha wananchi wanaohamishwa katika maeneo yanayolengwa kuwekezwa miradi ya maendeleo, wanahamishiwa katika maeneo mengine kwa ajili ya makazi pamoja na kupatiwa majengo yote ya huduma za kijamii, ikiwemo, misikiti, skuli, vituo vya Afya, masoko na kadhalika.

Aidha, Dk. Mwinyi alipata fursa ya kuutembea msikiti na madrasa hiyo na kuona maeneo mbali mbali.

Mapema, Waziri wa Maji na Nishati Suleman Masoud Makame aliwapongeza wananchi wa kijiji cha Dundua kwa kukubali kuondoka katika neo lao la asili na kupisha uendelezaji wa mradi mkubwa wa maendeleo na hatimae kupata makaazi bora.

Amewakata wananchi hao kuutunza msikiti na madrasa hiyo na kutumika kwa mujibu wa miongozo mema.

Nae, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab alisema hatua ya ufunguzi wa msikiti na madrasa hiyo unashabihiana na miongozo ya Mtume Muhamad (SAW) katika kuiendeleza dini ya Kiislamu, akibainisha madrasa hiyo ni kituo muhimu katika kuiendeleza dini hiyo.

Nae, Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwataka waumini na viongozi wa  msikiti huo kujiepusha na migogoro isiyo na lazima na kubainisha umuhimu wa kutumia busara katika uendeshaji wake na kuzingatia uwepo wa wazee.

Alishauri kuwepo Kamati ambapo pamoja na mambo mengine itasimamia kikamilifu masuala ya kijamii pamoja na harakati mbali mbali, ikiwemo mapambano dhidi ya udhalilishaji pamoja na matumizi ya dawa za kulevya.

Wakati huo huo; RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliendelea na utaratibu wake wa kuandaa futari kwa ajili ya wananchi wa Mikoa mitano ya Zanzibar.

Katika hafla ya futari kwa Wananachi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja iliofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ziliopo Mkokotoni, Dk. Mwinyi aliwashukuru wananchi wa Mkoa huo kwa kuitikia wito wake na kukutana pamoja kwa ajili ya futari, akibainisha kuwa  hilo ni jambo jema.

Aidha, aliwashukuru wananchi hao kutoka makundi mbali mbali kwa kumtunukia zawadi mbali mbali, jambo lililompa faraja kubwa na kuwaombea kheri kwa Mwenyezi Mungu.

Nae, Mkuu wa Mkoa huo, Ayoub Mohamed Mahamoud, alimshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa uungwana wake wa kuamua kuwafutarisha wananchi wa Mkoa huo, pamoja na kumuomba kupokea zawadi mbali mbali kutoka kwao.

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 

 E-mail: abdya062@gmail

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »