MKUU WA WILAYA YA KONGWA SELEMAN SELELA AMESEMA TASNIA YA HABARI INA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUIBUA CHANGAMOTO ZA JAMII.

MKUU WA WILAYA YA KONGWA SELEMAN SELELA AMESEMA TASNIA YA HABARI INA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUIBUA CHANGAMOTO ZA JAMII.

Mkuu huyo wa wilaya amebainisha hayo leo Mei 8,2021  katika maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya Habari mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Klabu ya  Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma[CPC] kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania [UTPC],Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa[TANAPA]pamoja na mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma[DUWASA].

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge ,mkuu huyo wa wilaya amesema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi  huku pia akiwataka wanahabari kuendelea kuwa na ubunifu katika uchakataji wa habari .

Katika hatua nyingine Selela amewataka wanahabari kwendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kuhakikisha wanaandika habari zenye mizania[balance]ili kuweza kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.

Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa  Dodoma [CPC]Musa Yusuph ameainisha changamoto zilizopo katika tasnia ya   habari ni pamoja na ubaguzi wa baadhi ya taasisi za serikali kuita vyombo vya habari kuelezea mambo nyeti ya kitaifa huku Katibu wa klabu hiyo Ben Bago akiwaasa baadhi ya maafisa habari serikalini kuacha tabia ya  kutoa lugha isiyokuwa na staha kwa wanahabari pindi wanapotekeleza majukumu yao.

Afisa Mhifadhi mkuu Mamlaka ya Hifadhi Tanzania[TANAPA]Jully Lyimo pamoja afisa utalii mkoa wa Manyara Cecilia Mkwabi wamelezea mchango wa Habari katika sekta ya utalii nchini.

Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yalifanyika Mei 3,2021  ambapo mkoa wa Dodoma yakifanyika Mei,8,2021 yakienda sambamba na kaulimbiu isemayo Habari kwa maufaa ya umma  ambapo tuzo zimetolewa kwa taasisi zilizo na ushirikiano mkubwa kwa tasnia ya Habari kuwa ni TANAPA  na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma [DUWASA  na Mwanachama bora wa mwaka akiwa ni Sebastian Warioba huku tuzo iliyokwenda kwa afisa habari mwenye ushirikiano mzuri ni Innocent Lupenza kutoka TANESCO.

Na Barnabas kisengi Dodoma Mei 08 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »