UKATILI WA KINGONO WAONGEZEKA KWA KASI KILOMBERO.

UKATILI WA KINGONO WAONGEZEKA KWA KASI KILOMBERO.

MATUKIO ya ukatili wa kingono yameripotiwa kuongezeka wilayani Kilombero mkoani Morogoro ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu kati ya Januari na Machi mwaka mwaka huu, jumla ya watoto 57 wamefanyiwa ukatili tofauti ikiwemo ulawiti, ubakaji na mimba za utotoni.           Hayo yalibainishwa jana na ofisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya Mlimba,

MATUKIO ya ukatili wa kingono yameripotiwa kuongezeka wilayani Kilombero mkoani Morogoro ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu kati ya Januari na Machi mwaka mwaka huu, jumla ya watoto 57 wamefanyiwa ukatili tofauti ikiwemo ulawiti, ubakaji na mimba za utotoni.          

Hayo yalibainishwa jana na ofisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya Mlimba, Latifa Kalikawe katika hafla ya maadhimisho ya kutambua uwezo wa mtoto wa kike katika masomo darasani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Plan International Tanzania.

Alisema idadi ya matukio hayo yameleta picha mbaya kwa halmashauri ambapo kati ya watoto hao 57, waliobakwa ni watoto 21, ulawiti watoto 5 na mimba watoto 31 ambapo hali hiyo pia inaonesha ni matokeo ya watoto kuanza kuzitambua haki zao na mahali sahihi pa kuripoti changamoto zao.

“Ni kweli kiwango cha ukatili kimezidi kuongezeka kakini elimu inazidi kuwafikia watoto na ndiyo maana takwimu zinazidi kuongezeka, maana watoto wanaanza kutoa taarifa katika maeneo husika hasa polisi kama sheria ya mtoto ya mwaka 2009  inavyotaka kwamba matukio  ya ukatili kama haya yaripotiwe katika kituo kikuu cha polisi cha wilaya’’alisema Kalikawe.

Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la plan International ofisi ya Ifakara wilaya ya kilombero bi Roda Msagila alisema katika kusaidia serikali kukabiliana na na changamoto hiyo shirika lilianza kutekeleza mradi wa kutoa elimu kwa watoto wa kike kuhusu kuijitambua kwa njia ya kuunda vikindi vya watoto (clubs) za kupinga ukatili

Alisema kuwa uundwaji wa vikundi hivyo hasa kwa wanafunzi wa Shule za msingi imesaidia kwa kiasi kukubwa kuwajengea watoto ujarisi wa kutoa taarifa na kuwafichua wale wanaokutana na madhira na namna hiyo na kiwezesha hatua mbalimbali za kisheria kuchukuliwa.

“Tuliamua kuunda club za watoto katika shule za msingi  ili kuwajengea watoto uwezo wa kujiamini wenyewe na kujua haki zao na maeneo ya kupeleka shida zao kwasababu awali walikuwa wanaogopa kufanya hivyo kwasababu kutishiwa na watu wabaya ambao walikuwa wanatekeleza hivyo wakijua ni makosa” Alisema Roda

Kadharika Alisema pamoja na Mambo mengine shirika limetoa vifaa mbalimbali vya kuwawezesha watoto hao kushiriki vizuri masomo yao ambayi ni boksi 725 za taulo za kike, mabegi na madaftari kwa wanafunzi wa kike waliofanya viziri kwenye masomo yao pamoja na vifaa vya michezo mipira na jezi vyenye thamani ya milioni 10.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »