TUMIENI MASOKO YA MADINI NCHINI KUUZA MADINI-WAZIRI BITEKO.

TUMIENI MASOKO YA MADINI NCHINI KUUZA MADINI-WAZIRI BITEKO.

Wachimbaji wa Madini wametakiwa kutumia masoko ya madiniyaliyoanzishwa kote nchini katika kuuza madini wanayozalishakatika migodi yao.Mwito huo umetolewa na Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko leotarehe 8 Mei 2021 wakati akifungua mafunzo kwa wachimbajiwadogo wa Madini Mkoa wa Geita.Waziri Biteko amewataka wachimbaji hao kujiepusha na utoroshajiwa madini, sambamba na kutoa taarifa pale wanapoona kunamchimbaji anakwenda


Wachimbaji wa Madini wametakiwa kutumia masoko ya madini
yaliyoanzishwa kote nchini katika kuuza madini wanayozalisha
katika migodi yao.
Mwito huo umetolewa na Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko leo
tarehe 8 Mei 2021 wakati akifungua mafunzo kwa wachimbaji
wadogo wa Madini Mkoa wa Geita.
Waziri Biteko amewataka wachimbaji hao kujiepusha na utoroshaji
wa madini, sambamba na kutoa taarifa pale wanapoona kuna
mchimbaji anakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na wizara
ya madini na serikali kwa ujumla.
Amewataka kuzingatia usalama mahala pa kazi pamoja na utunzaji
wa mazingira ili fedha wanayoipata kutoka kwenye madini
wanayozalisha kuitumia wakiwa na afya njema.
“Fuateni Sheria, Kanuni,  Taratibu na Miongozo inayosimamia
Sekta ya Madini ili kujiepusha na changamoto zinazoweza
kujitokeza ikiwemo kuwekwa kizuizini pindi wanapobainika
kujihusisha na utoroshaji wa wizi wa madini” Alikaririwa Mhe
Biteko
Waziri Biteko amesema kuwa lengo la msingi la kutoa mafunzo
hayo ni kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini nchini
kuwawezesha kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha ili
waweze kufanya uchimbaji endelevu na wenye tija. 
“Hii itachangia katika kuongeza uzalishaji kutoka kwa wachimbaji
wadogo na hivyo kuongeza mchango wao katika pato la Taifa
ambao kwa hivi sasa bado ni mdogo. 
Ndugu washiriki wa mafunzo, Nitoe rai kwenu kutumia vyema
fursa hii mliyoipata ya kukutana na wataalamu wa GST ili mjadili
kwa kina mambo yote yanayohusiana na mada kuu pamoja na
mambo mengine yanayolenga kuboresha kazi zenu za utafutaji,

uchimbaji na uchenjuaji wa madini wenye tija” Amesisitiza Waziri
Biteko
Amesema kuwa ni matarajio yake kuwa mafunzo hayo pamoja na
kitabu cha mwongozo yatawajengea uwezo ili kuendeleza ukuaji
wa Sekta ya Madini na kuongeza pato la Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel
ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa usimamizi
mzuri wa sekta ya madini na hivyo kusaidia utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi Kituo cha Uwekezaji
(EPZA) mkoani Geita.
“Geita imebadilika kutokana na madini, hata hapa tulipo ni
matokeo ya rasmilimali ya madini tuliyonayo ambapo mpango
wetu pia ni kulifanya eneo hili kuwa na huduma zote ili mwananchi
akija apate mahitaji yote muhimu” Ameeleza Mhe Gabriel.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa
Madini Tanzania (GST) Bi Yokbeth Muyumbilwa amesema kuwa
Taasisi hiyo imepitia mabadiliko mengi ya kimuundo ambapo
miongoni mwa majukumu yake ya msingi ni kusaidia wachimbaji
wadogo kwa kufanya utafiti na kutoa mafunzo ya kuboresha
uchimbaji na uchenjuaji wa Madini.

Na Mathias Canal, WazoHuru-Geita.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »