Jeshi la zimamoto na uokoaji linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi

Jeshi la zimamoto na uokoaji linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi

Jeshi la zimamoto na uokoaji nchini linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za jeshi hilo katika kutoa huduma za maokozi kutokana na vikwazo vinayotakana na jamii ikiwemo ujenzi holela wa makazi, uchache wa maafisa na askari vitendea kazi pamoja uhaba wa vituo vya zimamoto hapa nchini Kamishna Jenerali wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Tanzania

Jeshi la zimamoto na uokoaji nchini linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za jeshi hilo katika kutoa huduma za maokozi kutokana na vikwazo vinayotakana na jamii ikiwemo ujenzi holela wa makazi, uchache wa maafisa na askari vitendea kazi pamoja uhaba wa vituo vya zimamoto hapa nchini

Kamishna Jenerali wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Tanzania John Masunga Akizungumzia katika hitimisho la wiki ya  maadhimisho ya zimamoto yaliyofanyika mkoani Morogoro, amesema ujenzi holelea hasa maeneo ya mijini huchangia magari yao kutopitika kwa urahisi pamoja na kukosekana kwa maeneo ya kujazia maji kulingana na kasi ya mahitaji kwasasa.

Pia Kamishna Jenerali Masunga akaeleza mafanikio ya Jeshi hilo kwa kutoa eliu kwa jamii pamoja na vijana wa skauti katika shule za msingi na sekindari juu ya nana ya kutumia namba ya dharula pamoja na hudua ya kwanza

Akifunga maadhimisho hayo Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Khamis Hamza amesema lengo la serikali la kuanzisha Jeshi hilo ni kuokoa maisha ya watu sambamba na kutoa wito kwa jamii, viongozi wa serikali, Dini na vyama siasa kushirikiana katika kutoa elimu ya kuepuka ujenzi usiozingatia mpangilio wa miji.

Naye Mkuu wa Skauti Tanzania Mwantumu Mahiza akaeleza matunda yaliyopatikana  juu ya elimu hiyo katika kudhibiti matukio ya moto mashuleni

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »