DUNIANI SIO MAHALI SALAMA KAMA UNAVYOONA WEWE DUNIA IMEJAA NGUVU ZA GIZA NA MAPEPO

DUNIANI SIO MAHALI SALAMA KAMA UNAVYOONA WEWE DUNIA IMEJAA NGUVU ZA GIZA NA MAPEPO

Na. Kadala Komba Dodoma Mchungaji Moses Mchiwa wa kanisa la Pentecostal Assemblies of God (P.A.G)Beroya Christian Center Kizota jijini Dodoma.Alisema Dunia sio sehemu salama Kama mnavyoona kwa macho ya nyama, Dunia imetawaliwa na uwovu mwingi Dunia imejaa Nguvu za Giza na mapepo alisema Dunia imetawaliwa na watu wabaya ambao hawataki kuona mtu amefanikiwa ukifanikiwa tu

Na. Kadala Komba Dodoma


Mchungaji Moses Mchiwa wa kanisa la Pentecostal Assemblies of God (P.A.G)Beroya Christian Center Kizota jijini Dodoma.Alisema Dunia sio sehemu salama Kama mnavyoona kwa macho ya nyama, Dunia imetawaliwa na uwovu mwingi Dunia imejaa Nguvu za Giza na mapepo alisema Dunia imetawaliwa na watu wabaya ambao hawataki kuona mtu amefanikiwa ukifanikiwa tu wanaanza kukupiga vita.


Alisema mpendwa nakusihi kuanzia leo tembea na Neno la Mungu Neno la Mungu ni taa Soma katika kitabu Cha Zaburi 119:104.105 maandiko matakatifu yanatukumbusha Kwamba ukilishika Neno na kutembea na Neno utakapita gizani Neno litakuangazia, Hekima yako itakusaidia Kukaa uweponi mwa Mungu Hekima yako itakusaidia kutembea na Neno la Mungu,Hekima yako itakusaidia Mungu atembee na wewe wakati wote Bwana Yesu Asifiwe Maandiko yanatuongezea Nguvu na uwezo wa kuweza kufahamu Mambo kwa uwazi zaidi tuliyo pangiwa hapa Duniani alisema Soma Zeburi 119:98:101 Alisema mchungaji Mchiwa.

Hayo yamejili jumapili hii 23/5/2021  katika kanisa Hilo wakati wa ibada ya kusifu na kuabudu mkoani hapa.


Aidha Mchungaji Mchiwa Alisema ili tufanikiwe katika maisha yetu tunaitaji kutii Neno la Mungu sema Amina kumbukumbu la Torati ni kitabu kilichoandikwa na Musa Bwana Yesu Asifiwe , na hapa ili ufanikiwe katika maisha yoyote Yale unayotaka kuishi, Kama unataka kufanikiwa kibiashara,unataka upate watoto upate Mume utake jambo lolote unalotaka kufanya ili ufanikiwe ni vizuri ukatii Neno la Mungu mpendwa , Tujifunze kwa watu walio Tii Musa aliwapa ahadi  Wana wa Israel ikiwa Atatii Neno la Mungu watafanikiwa Soma Kumbukumbu la Torati  29:9 Yoshua 1:6.9 haya ni maandiko yanayotupa ujasiri.

Bwana Yesu Asifiwe Wana wa Mungu kumbe tunakumbushwa kuto kutenda Dhambi maana Ukifanya Dhambi inasababisha mapigo  unaweza kupigwa na Adui zako Kama utatenda Dhambi, sio kupigwa tu unaweza kuwasababishia watu wa Karibu yako kupigwa kwa Dhambi zako wewe, Lakini Kama utamtegemea Mungu kwenye maisha yako utafanikiwa Kiroho na kimwili Alisema mchungaji Mchiwa.

Kwaupande wake Mzee wa kanisa kiongozi wa kanisa Hilo Naftali Chibinda Alisema ni wakati wa Mungu kuzungumza na wewe mpendwa unatakiwa kuwa mnyenyekevu mbela za Mungu ujui kesho yako ili Mungu aseme na wewe nyenyekea , wakati huu Mungu yupo Karibu yako ili kukuhudumia sema na Moyo wako fungua Moyo wangu mkaribishe Bwana Halleluyah  Mungu unayetupenda kuliko sisi tunavyokupenda wewe, Unalo Neno kwa Jili ya kila mmoja wetu hapa usitupite Mokozi Sema Amen Alisema.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »