Kamati ya Wilaya ya ulinzi wa Wanawake na Watoto Wilayani Mpwapwa imeridhishwa na mwenendo wa huduma zinazotolewa kwa wanawake gerezani hapo.

Kamati ya  Wilaya ya ulinzi wa Wanawake  na Watoto Wilayani Mpwapwa imeridhishwa na mwenendo wa huduma zinazotolewa kwa wanawake gerezani hapo.

Kamati ya  Wilaya ya ulinzi wa Wanawake  na Watoto Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma imetembelea Gereza la Wanawake Wilayani Mpwapwa  na kuridhishwa na mwenendo wa huduma zinazotolewa kwa wanawake gerezani hapo.Baada ya kutembelea Gereza hilo leo  Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Mpwapwa  Paulo Sweya  amesema wameridhishwa na Mazingira Mazuri

Kamati ya  Wilaya ya ulinzi wa Wanawake  na Watoto Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma imetembelea Gereza la Wanawake Wilayani Mpwapwa  na kuridhishwa na mwenendo wa huduma zinazotolewa kwa wanawake gerezani hapo.
Baada ya kutembelea Gereza hilo leo  Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Mpwapwa  Paulo Sweya  amesema wameridhishwa na Mazingira Mazuri katika Gereza na namna ambavyo wanawake wanahudumiwa hasa katika kupatiwa haki zao za Msingi kama wanawake.


Jfive tv online imezungumza na  Mrakibu Msaidizi wa Magereza na Mkuu wa Gereza sehemu ya  Wanawake Veronica Mwasalemba amesema mwanamke anapoingia gerezani husitiriwa vyema bila ya kumvunjia haki zake huku akisema Kuwa wanawake wanaofungwa huacha pengo kuwa katika familia kwani husababisha hata watoto aliyowaacha kuishi bila ya kuwa na uangalizi mzuri.


Kwa upande wa Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpwapwa Mhe Lusajo Mutua akizungumza na J five one line tv blog amesema jamii inaweza kukosa picha kwanini mwanamke amepata adhabu na kusema Kuwa  huenda hupata nafasi ya kujitetea lakini kutokana na uoga  husababisha kushindwa kujitetea  na hapa anafafanua zaidi


Mmoja wa wanawake ambaye anatumikia kifungo  Cha miezi minne gerezani  ( jina lake limehifadhiwa)  mwenye watoto saba amesema  alifungwa kutokana na kupishana kauli na mama Mkwee  wake hali iliyopelekea kufungwa kwa miezi hiyo.



Shirika la Jukwaa la utu wa mtoto wilaya ya mpwapwa Children’s Dignity Forum CDF kwa ufadhili wa Comic Relief kupitia mradi wa Haki ya Binti  wamewezesha  kikao cha robo mwaka cha kamati hiyo ambayo imekuwa ni msaada mkubwa katika kuwasiadia wanawake na watoto pindi wanapokumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya Vitendo vya ukatili dhidi yao na wametoa Masada wa taulo za kike kwa wafungwa wanawake waliopo gerezani hapo. 

Na Barnabas kisengi Mpwapwa 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »