RPC Dodoma kufa na wahalifu Mtumba

RPC Dodoma kufa na wahalifu Mtumba

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  Kutokana na wimbi la uhalifu wa kutumia silaha kuzidi Katika kijiji Cha Mtumba Mkoani hapa ,baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho ambacho ndipo palipojengwa Mji wa Serikali wameliomba jeshi la Polisi Mkoani hapa kuingilia kati suala hilo huku wakiomba ulinzi wa ziada kwa wanawake na watoto ambao ndiyo wanaohujumiwa zaidi.Wakiongea na J

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

Kutokana na wimbi la uhalifu wa kutumia silaha kuzidi Katika kijiji Cha Mtumba Mkoani hapa ,baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho ambacho ndipo palipojengwa Mji wa Serikali wameliomba jeshi la Polisi Mkoani hapa kuingilia kati suala hilo huku wakiomba ulinzi wa ziada kwa wanawake na watoto ambao ndiyo wanaohujumiwa zaidi.
Wakiongea na J five Online tv kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Kijiji Cha Mtumba walisema kwa takribani miezi mitatu wamekuwa wakiishi kwa hofu Kama wako ugenini kutokana na Kijiji hicho kuvamiwa na watu wanao fanya ukatili kwa wanawake na watoto .
Hatua hii imekuja siku chache baada ya Mtoto mmoja mkazi wa Kijiji hicho ambaye pia ni Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Mtumba kubakwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kisha kumkata mapanga na kumtelekeza akiwa hajitambui.

John Joel alisema”Mimi na familia yangu tumehamia hapa hivi karibuni kama miezi sita iliyopita ,mwanzoni hali ilikuwa shwari lakini kwasasa naweza kusema tupo kwenye vita,hatujui kesho yetu inakuwaje kwani tunashindwa kufanya kazi kwa uhuru”alisema na kuongeza;
Tunaishi kwa hofu lakini zaidi tuna wasiwasi na watoto wetu,tutawaficha wapi,mana Sasa hata ukimtuma dukani unaogopa tunakuombà jeshi la polisi liiingilie kwa undani suala hiii,”alisema.
Naye Naomi Kuziganika alilieleza gazeti hili kuwa watu hao Wenye Nia ovu huwavamia watu wanaoenda kazini majira ya alfajiri na kuwapora mali walizonazo kisha kuwakata mapanga.


Almesema,wanawake wajawazito pia ni wahanga wa uhalifu huo ambapo wahalifu hwafuatilia na kuwakata mapanga bila sababu yoyote.
“Nadhani Sasa ni wakati ambao Jeshi la Polisi linapaswa kuwa macho zaidi, Kutokana na Jiji la Dodoma kuwa makao makuu visa vya uhakifu vinaongezeka,tunaishi jirani na mji wa Serikali ambapo wafanyakazi wengi wanaofanya kazi pale tunaishi nao hapa Mtumba,wanavamiwa wakiwa wanaenda kazi na kuwarudisha nyuma kiuchumi,”amesema.


“Inaonekana watu hawa wamewalenga zaidi wanawake na watoto,Matukio mengi yanawahusu wanawake na watoto,hata tukio la juzi Kuna msichana alikuwa anaenda kazini alipolwa simu na mkoba Kisha kupigwa mpaka akapoteza fahamu,”ameseema.


Kutokana na hayo Jeshi la  polisi mkoa wa Dodoma limewaonya wakazi wa Mtumba wanaojihusisha na uhalifu huku  likiwatoa hofu wakazi wa Mtumba Jijini hapa kuwa litaendelea kuwasaka wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na kusababisha watu kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji kwa hofu ya kuuawa.
Akiongea na J five Online tv katika mahojiano Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto ameseema jeshi hilo linapambana kufa na kupona  kuhakikisha wale wote waliofanya ukatili huo wanakamatwa na kufishwa kwenye vyombo vya dola kujibu tuhuma zinazowakabili.
“Tunazo taarifa za Mwanafunzi huyo ambaye alibakwa na kukatwakakwa mapanga na watu tunaowadhani kuwa ni majambazi,kwa Sasa binti huyo amelazwa katika hospitali ya Rufaa Dodoma kwa matibabu zaidi,”amesema Muroto


Licha ya hayo Kamanda Muroto amesema Jeshi hilo halitachoka kuwabaini wale wote wavunjifu wa amani na kuwataka washukiwa hao kujikita kufanya biashara na shughuli nyingine zitakazo wainua kichumi kuliko kuendelea kukatili maisha ya watu.
“Kuna watu wanashangaza Sana,badala ya kufanya kazi wao wananyang’anya ,niwaambie tu tumeshaanza kazi huko Mtumba na hivi karibuni tutawabaini waliohusika na tukio la kumbaka Mwanafunzi na uhalifu mwingine,tunataka jamii salama ili shughuli nyingine ziendelee,”amesema.


Hivi karibuni Katika kijiji hicho wakazi wengi wamekuwa wakilalamika kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi kwa Uhuru kutokana na Matukio mengi ya kubakwa na kupigwa na watu wasiofahamika hali inayozua taharuki kila kukicha.
Aidha uchunguzi mdogo uliofanywa na J five one line tv blog umebaini kuwa Katika kijiji hicho ifikapo majira ya saa 12 jioni  baadhi ya watu hujifungia ndani kuhofia kufikiwa na watuhumiwa hao na kuwadhuru.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »