TIMU YA TAIFA (WANAUME) WAVU WA UFUKWENI, KUSHIRIKI KOMBE LA AFRIKA NCHINI MOROCCO, KUTAFUTA NAFASI YA KUSHIRIKI MICHEZO YA OLIMPIKI 2021.

TIMU YA TAIFA (WANAUME) WAVU WA UFUKWENI, KUSHIRIKI KOMBE LA AFRIKA NCHINI MOROCCO, KUTAFUTA NAFASI YA KUSHIRIKI MICHEZO YA OLIMPIKI 2021.

Chama cha Mpira wa Wavu Nchini – TAVA, Tunayo furaha kuufahamisha uma kuwa timu yetu ya Taifa ya wannaume ya wavu wa ufukweni, imeingia kambini rasmi Jumatatu tarehe 7/6/21 Katika Hotel ya Golden Park ilioko Sinza, kumekucha, na itaanza mazoezi yake rasmi siku ya jumatano tarehe 9/6/21 katika fukwe za AZURA mjini Dar es salaam.

Lengo ni kujiandaa na Kombe la Afrika, litakalo fanyika mji wa Agadir, Nchini Morocco, Juni 21 – 28, 2021, kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Olimpiki, itakayo fanyika Tokyo, Japan 2021. Timu inatarajiwa kuondoka nchini Juni 19, 2021.

Ikumbukwe timu hii ilifanya vizuri hatua ya awali, shindano la kanda ya tano, liliofanyika Entebe, Uganda Disemba 2019, kwa kushinda mechi zake zote na kupata nafasi ya kusonga mbele kama vinara katika hatua ya mwisho kombe la Afrika. Aidha shindano hili lilikuwa lifanyike mwaka jana 2020 na kuhairishwa kwa sababu za mlipuko wa covid – 19.

Kikosi cha timu ya taifa kinaundwa na timu ya kwanza David Neeke na Ford Edward na timu ya pili Ezeckiel Rabson na Joseph Mafuru. Timu zote zitaendelea kunolewa
na Kocha Alfred Selengia ambaye ni mkufunzi wa makocha wa wavu wa ufukweni wa Shirikisho la mpira wa wavu Barani Afrika – CAVB.
TAVA inawaomba wadau, wafanya biashara na makampuni mbalimbali kusaidia kwa hali na mali timu hii ili iweze kujiandaa, kushiriki na kufanya vizuri.

Tunashukuru kwa ushirikiano na dhamira njema ya kuendeleza mchezo wetu Nchini.

Patrick MLOWEZI.
MWENYEKITI – TAVA.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »