WAZIRI MKENDA AITAKA TFRA KUANDAA MKAKATI WA UPATIKANAJI WA MBOLEA KWA BEI NAFUU.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021. Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe akisisitiza

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021.

.

sehemu ya Maafisa wa Serikali kutoka Wizara ya Kilimo na TFRA wakifuatilia kikao kazi kilichongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda wakati alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021. 

Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imetakiwa kuanisha mkakati wa upatikanaji wa mbolea nchini kwa bei nafuu.

 Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ametoa rai hiyo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea taasisi hiyo kujionea hali ya utendaji na upatikanaji wa mbolea wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam.


Pamoja na kuandaa mkakati wa urahisishaji wa upatikanaji wa mbolea, Pia Waziri Mkenda ameitaka taasisi hiyo kuandaa mkakati wa uanzishwaji wa viwanda vipya vya mbolea ili kuongeza uzalishaji wa pembejeo hiyo hapa hapa nchini.


Waziri Mkenda, amesema Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea, ina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa uzalishaji wa ndani wa mbolea, unapewa kipaumbele na kwa kuongeza uanzishwaji wa viwanda vipya; mbolea itakuwa ikipatikana kwa urahisi, nafuu na kila Mkulima atamudu kuinunua na kuitumia.


Prof Mkenda ameongeza kuwa Bodi na Menejimenti ya TFRA ibuni mkakati wa namna bora ya kuongeza uwekezaji hapa hapa nchini, kwa kuwa hilo ndiyo suluhisho la kweli katika kuwahakikishia Wakulima wengi wadogo unafuu bei.


Kadhalika, amewataka Watumishi wa TFRA kuongeza udhibiti kwenye usimamizi wa ubora wa mbolea hususan kwenye mikoa yenye matumizi makubwa ya mbolea.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »