Na Barnabas Kisengi-Dodoma Mwenyekiti kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la kusini Mwa Tanzania Mch. Mark Walwa Malekana ametoa wito kwa vijana kuwa na mpango mkakati wa wa kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuachana na dhana ya utegemezi kutoka kwa wazazi. Mchungaji Malekana amebainisha hayo leo Juni,12,2021 katika mwendelezo wa mkutano wa shangwe
Na Barnabas Kisengi-Dodoma
Mwenyekiti kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la kusini Mwa Tanzania Mch. Mark Walwa Malekana ametoa wito kwa vijana kuwa na mpango mkakati wa wa kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuachana na dhana ya utegemezi kutoka kwa wazazi.
Mchungaji Malekana amebainisha hayo leo Juni,12,2021 katika mwendelezo wa mkutano wa shangwe katika njia Yake ,Kizota Net,Event,2021 ambapo amesema pamekuwepo na kasumba kwa baadhi ya vijana kuwa na uvivu na kutegemea kwa wazazi ambao ni wazee hivyo ni wakati sasa umefika kwa vijana kufanya kazi kwa bidii.
Aidha,Mchungaji Malekana ametoa hamasa kwa kwa vijana na watanzania kwa ujumla kuacha anasa na kujikita zaidi kufanya mambo yampendezayo Mungu pamoja na kuhimiza uvaaji wa nguo za maadili .
Kuhusu suala la uimbaji kanisani,Mchungaji Malekana ametoa wito kwa kwaya zilizo ndani ya kanisa la Waadventista Wasabato kuimba kwa kufuata kanuni za uimbaji ndani ya kanisa huku akitumia fursa hiyo kuipongeza kwaya ya Sauti Jangwani kutoka Mkoani Shinyanga kwa kuelendelea na uimbaji mzuri huku pia akiwaasa vijana waliopotea kwa kujikita katika dawa za kulevya,uasherati kurejea kwa Yesu Kristo kwani yeye ndie Mwokozi wa kweli.
Katika Sabato ya leo Juni 12,2021 Jumla ya watu 47 wamebatizwa kwa maji mengi baada ya kukiri na kumwamini Yesu kristo kuwa mwokozi katika maisha yao ambapo wamesema kanisa la Waadventista Wasabato ulimwenguni linasimamia misingi bora na ukweli kuhusu biblia ndio kivutio kiuu kwa kubatizwa .
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *