TANZANIA YAENDELEA KUPATA NEEMA KUPITIA UTALII BARA LA AFRIKA,

TANZANIA YAENDELEA KUPATA NEEMA KUPITIA UTALII BARA LA AFRIKA,

-Mkutano ujao wa UNWTO kwa Bara la afrika kufanyika Tanzania Na Mwandishi Wetu, Windhoek, Namibia. UJUMBE wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damasi Ndumbaro ambao upo mjini hapa kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia masuala ya Utalii Duniani [UNWTO], ambao ni mahususi kwa nchi za Kiafrika kueweza

Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Kimtaifa la Utalii (UNWTO) ulioanza Juni 14, 2021 Jijini Windhoek nchini Namibia, Mkutano huo una lengo la kukabiliana  na athrai za UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na baadhi ya Mawaziri wa utalii kutoka nchi mbalimbali  za a Afrika  wakimfuatilia  Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob wakati akifungua rasmi Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) ulioanza  Juni 14,  Jijini  Windhoek nchini Namibia, Mkutano huo una lengo la kukabiliana na athari za UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali.
Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii ( UNWTO), Zurab Pololikashvili akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob ambapo amesema moja ya kipaumbele chake ni kuhakikisha nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania ambazo zina vivutio vingi na vya kipekee zinajengewa uwezo katika suala la kutangaza vivutio vya utalii ilivyonavyo ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Watalii
Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara, Beatrice Kessy kutoka TANAPA akiwa na  baadhi ya Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakimfuatilia Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob wakati akifungua rasmi Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) ulioanza jana  14,  Jijini  Windhoek nchini Namibia, Mkutano huo una lengo la kukabiliana na athari za UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali.
Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akizungumza wakati akifungua  rasmi Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii (UNWTO) ulioanza jana Juni 14, 2021 Jijini Windhoek nchini Namibia, Mkutano huo una lengo la kukabiliana  na athariza UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali ambapo amezitaka nchi za Afrika kuungana kwa pamoja kutangaza vivutio vya utalii ili kuondokana na dhana kuwa  Afrika ni bara la Njaa, Vita na Maradhi.
Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akiwa amesimama na baadhi ya viongozi wakati wa kuimba wimbo wa taifa wa taifa hilo kabla  ya kufungua rasmi Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Kimtaifa la Utalii (UNWTO) ulioanza  Juni 14, 2021 Jijini Windhoek nchini Namibia, Mkutano huo una lengo la kukabiliana  na athari za UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali. Wa pili kullia kwake ni  Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvili na wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Utalii, Mazingira na Misitu wa Namibia, Mhe. Heathar Sibungo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akioneshwa  picha mjengeo  (video) ya wimbo wa ”Kwangaru remix” ya   Mwanamuziki Mashuhuri nchini Tanzania, Rajab Kahali anayejulikana kwa jina la Harmonize na Wafanyabiashara wa bidhaa za  Utalii wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika  Jijini Windhoek nchini Namibia, ambapo wamesema wanampenda sana Mwanamuziki huyo kutoka na tungo zake za nyimbo zinazogusa nyoyo za mashabiki wake. 
Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri wa Utalii wa nchi mbalimbali za Afrika mara baada   ya kufungua rasmi Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Kimtaifa la Utalii (UNWTO) ulioanza  Juni 14, 2021 Jijini Windhoek nchini Namibia, Mkutano huo una lengo la kukabiliana  na athari za UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali. Wa kushoto kwake ni  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro

-Mkutano ujao wa UNWTO kwa Bara la afrika kufanyika Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Windhoek, Namibia.

UJUMBE wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damasi Ndumbaro ambao upo mjini hapa kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia masuala ya Utalii Duniani [UNWTO], ambao ni mahususi kwa nchi za Kiafrika kueweza kujadili na kufanya tafakuri kwa jinsi gani sekta ya Utalii itakavyorejea kwenye mstari wake baada ya kushambuliwa na madhara ya ugonjwa wa UVIKO 19, ambapo Tanzania mkutano ujao imekubaliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Waziri Mhe. Ndumbaro amesema kuwa, ujumbe wa Tanzania umeweza kupata faida mbalimbali  sambamba na kupata uzoefu mkubwa ikiwemo pia kutangaza fursa za utalii wa Tanzania katika mkutano huo ambao una aatalaamu Wabobezi Utalii Duniani

‘’Tumekutana nchi nyingi za Kiafrika, tumejadili mambo mengi, tumebadilishana uzoefu mkubwa tumepata mawasilisho mbalimbali kutoka kwenye makampuni ambayo yana uwezo wa juu kabisa wa kutangaza utalii Duniani.

Lakini pia tumepata fursa ya kufanya vikao vya ana kwa ana na wadau mbalimbali moja kati ya wadau hao ni Katibu Mkuu ambaye anayeshughulikia masuala ya Utalii wa umoja wa Mataifa, Zurab Pololikashvili,  tumezungumza  naye vizuri kabisa na pia amekubali mkutano ujao wa utalii Barani Afrika ufanyikie Tanzania’’. Alisema Mhe. Ndumbaro.

Mhe. Ndumbaro ameongeza kuwa, Katibu huyo pia amekubali yeye mwenyewe binafsi kutembelea Tanzania na kuonana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa pamoja na wadau wa utalii kwa ajili ya kufanya maongezi juu ya mustakabali wa Utalii  baada ya UVIKO 19.

‘’Lakini muhimu zaidi, tumeweza kuomba na kukubaliwa kuiingiza Tanzania kuwa  moja kati ya nchi tatu barani afrika ambazo zitapata mradi wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya Utalii. Nchi zingine zikiwa Namibia na Cape Vede ambazo zimeshaingizwa toka zamani kwa namna ya kipekee Tanzania tumepewa upendeleo huo baada ya kushiriki hapa na tayari tutaingizwa katika mradi huo mkubwa…’’. Alisema Mhe. Ndumbaro.

Aidha, amesema Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umepata utaalam na uzoefu mkubwa kwa jinsi gani watakavyoweza kunasuka na ugonjwa huo wa UVIKO 19, amewapongeza watanzania kushiriki na kuweza kufanikiwa.

Katika mkutano huo, leo 16 Juni kutakuwa na  Mawaziri 15  kutoka nchi 15  za Afrika ikiwemo Tanzania wapata nafasi ya kuziongelea nchi zao katika mkutano ambao utarushwa moja kwa moja na televisheni mbalimbali za ndani na nje ya Namibia ikiwemo mitandao ya Kijamii.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »