Wadau wa kahawa nchini watakiwa kuzalisha kwa tija ili kuleta matokeo chanya katika soko la kahawa.

Wadau wa kahawa nchini watakiwa kuzalisha kwa tija ili kuleta matokeo chanya katika soko la kahawa.

Na Barnabas kisengi DODOMA  JUNE 17.2021. Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amebainisha kuwa  tija ndogo ndiyo inayosababisha kushuka kwa bei ya soko la kahawa  huku akiwataka Wadau wa kahawa nchini kuzalisha kwa tija ili kuleta matokeo chanya katika soko la kahawa. Hayo yamebainishw leo jijini Dodoma na mkuu wa mkoa huyo wa mkoa

Na Barnabas kisengi DODOMA 

JUNE 17.2021.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amebainisha kuwa  tija ndogo ndiyo inayosababisha kushuka kwa bei ya soko la kahawa  huku akiwataka Wadau wa kahawa nchini kuzalisha kwa tija ili kuleta matokeo chanya katika soko la kahawa.

Hayo yamebainishw leo jijini Dodoma na mkuu wa mkoa huyo wa mkoa wakati akifungua Mktano mkuu wa  11 wa wadau wa kahawa 2021 na kubainisha kuwa zao la kahawa ni miongoni mazao la kimkakati yaliyochaguliwa na serikali ili kuweza kutoa mchango mahususi katika jitiahada za serikali ikiwemo kutatua tatizo la ajira nchini.

Aidha, Mgumba amebanisha miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya kahawa nchini ni tija ndogo ,uzalishaji mdogo,kuyumba kwa bei katika soko la Taifa,ukosefu wa mitaji kwa wakulima kwa kushindwa kukopesheka kwenye Taasisi za fedha mambo ambayo yanasababisha kilimo cha kahawa kuonekana kuwa hakilipi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Aurelia Kamuzora amezungumzia umuhimu wa zao hilo huku akieleza jinsi wakulima wanavyolima ekari nyingi pasipo kufata kanuni za kilimo mwishoe wanavuna kidogo jambo ambalo linawarudisha nyumba katika uzalishaji.

Bodi ya kahawa Tanzania imeanzishwa kwa sheria namba 23 ya mwaka 2001 na marekebisho ya sheria ya bodi za mazao ya mwaka 2009 huku kongamano hilo likibebwa na kaulimbi isemayo ‘’uzalishaji wenye tija ndio nguzo ya maendeleo ya sekta ya kahawa’’.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »