OLE SABAYA AKANA MASHTAKA MAWILI ALIYOSOMEWA

OLE SABAYA AKANA MASHTAKA MAWILI ALIYOSOMEWA

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wamesomewa mashtaka mawili yanayowakabili kati ya mashtaka sita waliyonayo pamoja na wenzao watatu. Imeelezwa leo Ijumaa Juni 18, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa mashtaka mengine manne upelelezi wake bado haujakamilika. Wakili mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka amemweleza hakimu mfawidhi wa

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wamesomewa mashtaka mawili yanayowakabili kati ya mashtaka sita waliyonayo pamoja na wenzao watatu.

Imeelezwa leo Ijumaa Juni 18, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa mashtaka mengine manne upelelezi wake bado haujakamilika.

Wakili mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka amemweleza hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya, Salome Mshasha kuwa upande wa mashtaka umekamilisha upelelezi na upo tayari kuwasomea maelezo watuhumiwa.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Tarsila Gervas amesema Februari 9, 2021 katika mtaa wa Bondeni, Sabaya akiwa na watuhumiwa wenzake wawili walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kuvamia duka la Said Saad na kuwaweka chini ya ulinzi.

Gervas amesema Sabaya na walinzi wake, Sylivester Nyingu (26) maarufu Kicheche na Daniel Mbura(38) walitenda kosa hilo baada kumfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetini na kumuibia 390,000.

Katika tukio hilo wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao pia wanatuhumiwa kumpiga mateke kumtishia silaha na kumpora simu na Sh35,000 Ramadhani Ayoub. Watuhumiwa hao ambao walikana mashtaka yanayowakabili wanatetea na wakili, Moses Mahuna.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana walirudishwa mahabusu gereza kuu la Kisongo baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Julai 2, 2021.

Mashtaka mengine manne yanayowakabili watuhumiwa hao ni ya utakatishaji fedha, uhujumu uchumi, kuomba rushwa na kuunda genge la uhalifu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »