Rais Samia Suluhu Hassan, leo Juni, 25.2021 amezungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC.

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Juni, 25.2021 amezungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 25 Juni, 2021 amezungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na kueleza kuwa Taaisisi za Dini nchini ni muhimu kwa kuwa zina mchango mkubwa katika kudumisha amani, kustawisha maisha ya wananchi na kupambana na umasikini. Mhe. Rais Samia amewasihi Watanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu (TEC) Kurasini mkoani Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Jude Thaddeus Ruwa’ichi mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 25 Juni, 2021. Katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya ambaye pia ni Rais wa TEC Askofu Gervas Nyaisonga na wakwanza kulia ni Askofu Augustine Shao kutoka Jimbo Katoliki Zanzibar
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC katika ukumbi wa AMECEA Kurasini mkoani Dar es Salaam.
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini wakiwa wamesimama kushukuru mara baada ya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Makao Makuu ya TEC Kurasini Mkoani Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya ambaye pia ni Rais wa TEC Askofu Gervas Nyaisonga mara baada ya kupiga picha za kumbukumbu na Maaskofu wa TEC Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 25 Juni, 2021 amezungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na kueleza kuwa Taaisisi za Dini nchini ni muhimu kwa kuwa zina mchango mkubwa katika kudumisha amani, kustawisha maisha ya wananchi na kupambana na umasikini.

Mhe. Rais Samia amewasihi Watanzania kuendelea kuvumiliana kwenye tofauti za Kidini zinazojitokeza ili kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini. Amesema amani na utulivu nchini ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya taifa, hivyo ni vyema viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani kwa waumini wao.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewaomba Maaskofu na viongozi wengine wa Dini kuwakumbusha waumini wao kuhusu umuhimu wa kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Mhe. Rais Samia ametumia mkutano huo na Viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kueleza mipango ya Serikali ya miaka mitano kuwa ni pamoja na kudumisha mema yote ya Awamu zilizotangulia na kubuni mengine mapya.

Amesema Serikali imejipanga kuendeleza kukuza uchumi ili kupambana na umasikini na tatizo la ajira kwa kuboresha mazingira ya biashara.

Kwa upande wake Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga amemuhaklikishia Mhe. Rais Samia kuwa Baraza hilo litaendelea kushirikiana na Serikali anayoiongoza kwa lengo la kuwaletea Wananchi maendeleo.

Askofu Mkuu Nyaisonga amempongeza Mhe. Rais Samia kwa kupokea majukumu ya Urais na kuongoza Taifa kwa utulivu na amani. Kuonyesha nia thabiti ya kushirikiana na ulimwengu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Aidha, Askofu Mkuu Nyaisonga amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kutenga muda na kuwasikiliza ambapo ameelezea hatua hiyo ni kuonesha nia ya dhati katika kukuza taifa lenye mshikamano, maridhiano,na maendeleo ya kweli.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »