WANACHUO WA CHINA WATAKA WAKULIMA KURAHISISHIWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI.

WANACHUO WA CHINA WATAKA WAKULIMA KURAHISISHIWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI.

Wanafunzi wanaosoma chuo kikuu cha kilimo nchini China CAU wameiomba serikali ya mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na chuo hicho ambao wanatekeleza mradi wa pamoja wa kupunguza umasikini kwa wakulima wadogo kupitia kilimo cha mahindi kuangalia namna ya kuwapunguzia gharama wakulima hao ili kuendana na kipato chao Wanafunzi hao ambao wanasoma kwa njia ya mtandao

Wanafunzi wanaosoma chuo kikuu cha kilimo nchini China CAU wameiomba serikali ya mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na chuo hicho ambao wanatekeleza mradi wa pamoja wa kupunguza umasikini kwa wakulima wadogo kupitia kilimo cha mahindi kuangalia namna ya kuwapunguzia gharama wakulima hao ili kuendana na kipato chao

Wanafunzi hao ambao wanasoma kwa njia ya mtandao kutokana na changamoto ya usafiri iliyosabishwa na ugonjwa wa uviko 19, walitoa rai hiyo jana wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo mkoani humo kuangalia namna chuo hicho kinavyotekeleza miradi mbalimbali hasa kwa kusaidi wakulima masikini

Juliet Frank, mmoja wa wananfunzi hao alisema pamoja na mambo mengine mradi huo kuonesha kuwanufaisha wakulima wengi baada ya kupata elimu ya kilomo cha kisasa chenye kuwaletea tija lakini ipo haja ya wataalamu kuangalia namna bora ya ya kuwapunguzia kazi za uzalishaji

“pamoja na kwamba njia hii imewasaidia sana lakini kuna kila sababu ya kutafuta njia mbadala ya kuwasaidia hawa wakulima kupunguza mzigo wa kazi, japo hakuna njia rahisi katika kutafuta mafanukio lakini kukiwepo na vitendea kazi kama mashine za kupandia na kupalilia mahindi kama ilivyo katika mazao mengine itasaidia pia kuokoa muda” alisema

Naye Salma Shehe alisema kuwa njia nyingine ambayo itaweza kuwasaidi wakulima hao ni mradi huo kuondokana na kilimo cha msimu na kuanza kutumia kilimo cha uwagiliaji ambacho kimeonesha tija katika kipindi cha hivi karibuni hasa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Alisema mabadiliko ya tabia ya nchi yamekuwa yakiathiri kwa kiasi kikubwa wakulima wadogo ambao wamekuwa wakitegemea mvua pekee ambapo pindi mvua hizo zinapokosekana na kuzidi mazao mengi yamekuwa yakiharibikia shambani na kuwasabishai hasara

“kwa sababu lengo la mradi ni kusaidia wakulima wadogo kwa kutumia teknolojia ya kisasa pia wafikishiwe hata elimu ya kilimo cha umwagiliaji ili waondokane na kilimo cha msimu ambacho kinategemea mvua hasa huu ambao kuna mabadiliko tabia ya nchi” alisema

Awali Akielezea utekelezaji wa mradi huo Ernest Mkongo alisema kuwa mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2011 kwa kuanza na kijiji kimoja cha Peapea wilayani Kilosa kisha baadaye kuhamishiwa katika kijiji cha Mtegi wa simba halmashauri ya Morogoro mwaka 2014

Alisema kupitia mradi huo wakulima waliweza kujifunza njia za kisasa ambapo waliweza kuvuna hadi gunia 18 kwa hekari moja kulinganisha na awali ambapo walikuwa wanavuna gunia nne hadi tano kwa hekari moja

“teknolojia hii imesaidia kuongeza tija kwa kiasi kikubwa sana mara tatu  zaidi ya awali ambapo mkulima alikuwa anaambulia gunia tano pekee kwa hekari moja,  na kubwa zaidi elimu ile haikuishia kwa wanufaika wachache bali iliwafikia hadi wanakijiji wengine ambao walijifunza kupitia kwa wenzao” alisema

Aliongeza kuwa baada ya mafanikio katika majaribio hayo mradi ulipanuka na kuvifikia vijiji 8 kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Morogoro katika kipindi cha mwaka 2018 hadi mwaka 2021

Alivitaja vijiji vingine ni pamoja na Letugunya na Ngayaki vilivyopo Gairo, Kitete wilayani Kilosa , Kisegese Kilombero, Kiswago Malinyi,  Kikundi Morogoro, Makuyu Mvomero paoja na  Mwaya kilichopo Ulanga

Kwa upande wake afisa kilimo wandaizi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Gabishi Evance alisema mradi huo umeweza kuwafikia wakulima wadogo 1667 kwa wastani wa hekari moja katika vijiji vyote kumi ambapo mradi umepita

Alisea mbali na kufikia wakulima hao pia mradi unatarajiwa kuendelea kupanua wigo na kufikia wakulima zaidi ya 10000 mkoani humo sambamba na kuwafikia wakulima wengine ambao watajifunza kupitia kwa wenzao kwa njia ya elimu ya shamba kwa shamba

“tunaamini kadri mradi utakavyoendelea kukua utawafikia wakulima wengi zaidi na hata wale wakulima wengine ambao hawatofikiwa na mradi wataweza kujifunza kwa wenzao, kwasababu akiona mwenzake amelia heka moja akapata mavuno mengi naye atapenda kujifunza teknolojia hiyo na kujikuta ameondokana na umasikini” alisema

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »