Serikali Kuendelea Kuiunga Mkono Timu ya Riadha inayoshiriki Olimpiki.

Serikali Kuendelea Kuiunga Mkono Timu ya Riadha inayoshiriki Olimpiki.

Na Octavian Kimario,Arusha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul amesema kuwa Serikali inaendelea kuiwezesha timu ya Riadha  ili iweze kufanya vyema katika mashindano ya ndani na  Kimataifa.  Mhe. Gekul amesema hayo Julai 11, 2021 Jijini Arusha alipowakibidhi wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha bendera ya Taifa, vifaa vya michezo pamoja na tiketi

Na Octavian Kimario,Arusha

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul amesema kuwa Serikali inaendelea kuiwezesha timu ya Riadha  ili iweze kufanya vyema katika mashindano ya ndani na  Kimataifa. 

Mhe. Gekul amesema hayo Julai 11, 2021 Jijini Arusha alipowakibidhi wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha bendera ya Taifa, vifaa vya michezo pamoja na tiketi za ndege tayari kwa ajili ya kwenda   kwenye mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika nchini Japani mwezi Agosti, 2021.

“Macho yote ya Watanzania wapenda michezo yapo nyuma yenu yakiwatazama na kuwafuatilia kwa karibu kwa matumaini makubwa kwamba mtatuwakilisha vyema, mmepata muda wa kutosha kujifua na kujiandaa kwa zaidi ya miezi miwili, Serikali inaimani kubwa kwamba mtarejea na medali” amesema Mhe. Gekul

Naibu Waziri Mhe. Gekul pia amewahakikishia wachezaji hao kuwa, Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa inazisaidia timu za Taifa pamoja na Vyama vya Michezo na Mashirikisho ili ziweze kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Michezo ulioanzishwa ambapo 

amevitaka vyama pamoja na mashirikisho ya michezo  kuzingatia utawala bora pamoja na kuratibu mashindano katika ngazi za mikoa na Taifa ili kuibua wacheza mahiri.

“Serikali imedhamiria kwa dhati kuendeleza michezo hapa nchini, na katika kudhihirisha hilo Wizara kupitia BMT imesaidia maandalizi ya kambi ya Timu hii pamoja na stahili nyingine za wachezaji watakapo kuwa nchini Japan” amesisitiza  Mhe. Gekul.

Timu ya Taifa ya Riadha iko kambini jijini Arusha ikijiandaa kushiriki mashindano hayo ambapo  wachezaji watatu wamefanikiwa kufuzu viwango vya Olimpiki ambao ni Felix Simbu, Failuna Matanga na Gabriel Geay, na wanatarajia kuondoka nchini Julai 27, 2021 kuelekea nchini Japan  kwa ajili ya mashindano hayo.  

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »