SHEIKH WA DODOMA ATUMIA SWALA LA EID AL HAJJ KUWAASA WATANZANIA MAMBO MAKUU MATANO

SHEIKH WA DODOMA ATUMIA SWALA LA EID AL HAJJ KUWAASA WATANZANIA MAMBO MAKUU MATANO

Na Hamida Ramadhan, Dodoma SHEKHE wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu ameitumia Ibada ya swala ya Eid El Hajj kuwaasa watanzania katika mambo matano ikiwemo kuendelea kuilinda, kuienzi na kuikumbatia amani iliyopo na kujilinda na ugonjwa wa virusi  vya Corona.  Aidha Shekhe amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kwa kujilinda na ugonjwa wa Covid 19 na

Na Hamida Ramadhan, Dodoma


SHEKHE wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu ameitumia Ibada ya swala ya Eid El Hajj kuwaasa watanzania katika mambo matano ikiwemo kuendelea kuilinda, kuienzi na kuikumbatia amani iliyopo na kujilinda na ugonjwa wa virusi  vya Corona. 

Aidha Shekhe amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kwa kujilinda na ugonjwa wa Covid 19 na kuzitumia siku 10 kuendelea kutenda matendo mema ya kumpendeza Mwenyezimungu pamoja na kuitumia siku ya leo kuchinja na kula kwa pamoja na familia na watu wasiojiweza. 


Akizungumza leo Jumatano Julai 21 wakati wa ibada ya swala hiyo iliyofanyika katika Msikiti wa Gadaffi Jijini Dodoma Sheikhe Rajabu amesema amewaasa watanzania kuendelea kuilinda amani iliyopo.
“Watanzania tuendelee kuilinda amani iliyopo tumuenzi mama yetu Samia Suluhu Hassan na tukumbuke sisi ndio wakipelekaTanzania yetu mbele na ndio pia tutakaoitoa Tanzania yetukwenye viashiria vya uvunjifu wa amani ,” amesema Shekhe Mustapha. 
Akizungumzia suala zima la Ugonjwa wa Virusi vya Covidi 19 CORONA upo na tuendelee kujikinga mwanadamu hudai kujiua mwenyewe tunzingaitie masharti yanayotolewa na wataalamu wa afya 
Aidha shekhe Rajabu amewataka watanzania kuzingatia masharti yanayotolewa na watumishi wa afya kwa kunawa mikono mara kwa mara na kutumia vitakasa mikono ili kuzuia kuwaambuiza wengine na kujiambukize wenyewe .
“Ugonjwa  huu upo licha ya kutoenea  kwa kasi kubwa ndani ya nchi yetu lakini tukumbuke  kwamba kinga ni bora kuliko tiba hivyo tufuate masharti yanayotolewa na wataalamu wetu wa afya, ” amesema  Shekhe  Mustapha. 


Pia amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kutimiza ibada ya kuchinja kwa sadaka iliyo halali kama ilivyoandikwa na kuelekeza ndani ya vitabu vya dini ya Kiislamu. 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »