WAZIRI MKENDA AYATAKA MABENKI KUTOA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI

WAZIRI MKENDA AYATAKA MABENKI KUTOA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Na Barnabas Kisengi,Dodoma Waziri wa kilimo Prof ADOLF MKENDA amezitaka taasisi za kibenki hapa nchini  kuhakisha zinawapunguzia riba na kuwapatia mikopo kwa wakati wakulima na wafugaji pindi wanapokuwa wanahitaji mitaji katika shughuli za kilimo na mifugo ili kuhakikisha wakulima wanafaidika na kilimo chenye tija na kilimo biashara ambapo asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima. Kauli

Na Barnabas Kisengi,Dodoma


Waziri wa kilimo Prof ADOLF MKENDA amezitaka taasisi za kibenki hapa nchini  kuhakisha zinawapunguzia riba na kuwapatia mikopo kwa wakati wakulima na wafugaji pindi wanapokuwa wanahitaji mitaji katika shughuli za kilimo na mifugo ili kuhakikisha wakulima wanafaidika na kilimo chenye tija na kilimo biashara ambapo asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima.


Kauli ameitoa jiji dodoma wakati akifunga maonyesho ya wiki y Pass Trust iliyofanyika jijini dodoma kwa kuwanufaisha wakulima ambao baadhi yao wamefaidika na kupata zana za kilimo kama matrenkta kwa mkopo wa garama nafuu kwa kusimamiwa na na taasisi ya PASS TRUST ambayo iliandaa kongamano la wiki moja kwa wakulima 
“napenda pass trust kuhakikisha mnawekeza na kuwasaidia wakulima wa alizeti katika mikoa ya kimkakati mikoa ya simiyu,singida na dodoma hii ni mikoa ya kimkati katika kuhakikisha tunalima kilimo cha alizeti na kuwa modo hapa nchini kwakuwa tuna viwanda vingi vya kusindika alizeti ila kwa sasa maligafi imekuwa ndogo sasa nyinyi pass trust mkiwekeza hasa kuwasaidia wakulima wa mikoa hii mitatu kwa pembejeo na mitaji wakulima watafa8dika kwa haraka na muda mfupi na kutambua kuwa alizeti ni zao la kilimo chenye tija na kilimo biashara hapa nchini na kitaweze kuwashawishi kundi kubwa la vijana ambao wameanza kukata tamaa katika kilimo”alisisitiza Prof Mkenda.


Dkt TAUSI KIDA ni Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya PASS TRUSI  amesema anashukuru uongozi wa mkoa kwa kuandaa wiki hii ya maonyesho malimbali na mafunzo kwa wakulima ambapo yamewajengea uwezo mkubwa wakulima kuweza kubadilika
Aidha DKt  KIDA amesema pass imekuwa msaada mkubwa kwa wakulima kwa kuwajengea uwezo na kuwapatia misaada ya pembejeo na na zana za kilimo kwa wakulima wadogo,wakati na wakulima wakubwa na pia pass imekuea kiunganishi kwa wakulima na taasisi za kibenki ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazowakabili wakulima hapa nchini
“kuna wakulima zaidi ya milioni mbili wamenufaika na taasisi ya pass katika mikopo yenye riba nafuu na kuwadhamini katika taasisi za kibenki na sasa tunaandaa wakulima wa zao la alizeti ambalo ni zao la kimkakati katika mikoa ya simiyu,singida na dodoma hapa tutashirikiana na wakulima ili kuhakikisha tunawasaidia kupata pembejeo bora za muda mfupi ili waweze kuzalisha alizeti kwa wingi na kuhakikisha mikoa hii inazalisha alizeti nyingi na kuondokana na uhaba wa mafuta ambayo kwa sasa mafuta mengi yanaagizwa kutoka nje ya nchi”amesema Dkt KIDA.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa dodoma ANTONY MTAKA ametoa wito kwa vijana wa mkoa wa dodoma kuacha kusubiri ajira za serikalini na kwa sasa wajikite katika swala la kilimo kutoksna na kilimo licha ya kuwa kilimo ni uti wa mgongo sasa kilimo ni biashara hivyo vijana wakiwa wamejiunga katika vikundi yeye kama mkuu wa mkoa wa dodoma atawatafutia maeneo katika wilaya kutokana na mazao yanayoendana na hali ya hewa ya maeneo yao.
“pia nitahakikisha zao la alizeti na zabibu yanakuwa mazao mkakati katika mkoa wa dodoma na nyinyi taasisi ya pass nitawaomba sana ushirikiano wenu kuhakikisha mnawasaidia sana wakulima wa mkoa wangu wa dodoma katika kuwaelimisha juu ya zao la kilimo cha alizeti na zabibu na kuwapatia pembejeo bora na kuwapatia mikopo ya garama nafuu ili vijana wengi waweze kutambua kilimo ni biashara na sio kubweteka kutembea na vyeti kwenye bahasha wakisaka ajira ya serikali wakati sasa serikali imewekeza sana katika kilimo”


Wiki hii ya maonyesho na elimu ya wakulima iliandaliwa na pass truns ilizinduliwa Julai 22 2021 na waziri mkuu mstaafu MIZENGO PETER PINNDA na imehitimishwa kilele leo Julai 24 2021 na waziri wa kilimo Porf ADOF MKENDE ambapo baadhi ya wakulima wamekabidhiwa matrekta na zana za kilimo kwa kukopeshwa kwa garama nafuu ambapo waziri Prof MKENDA amewakabidhi vifaa hivyo tayari kwa kujishughulisha na shughuli za kilimo katika msimu ujao.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »