WAKULIMA WARIDHISHWA NA BEI YA ZAO LA PAMBA SIMIYU

WAKULIMA WARIDHISHWA NA BEI YA ZAO LA  PAMBA SIMIYU

Na Barnabas Kisengi, Simiyu Baadhi ya Wakulima wa zao la Pamba Wilayani Maswa mkoani Simiyu wakizungumza kwa nyakati tofauti na  Mtandao huu  ,akiwemo Diwani wa viti Maalum tarafa ya Sengerema, Maswa Julieth Mongo wamesema hali ya soko ya zao la pamba inaridhisha ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo bei ya zao hilo ni Tsh.1400 hadi 1500

Na Barnabas Kisengi, Simiyu

Baadhi ya Wakulima wa zao la Pamba Wilayani Maswa mkoani Simiyu wakizungumza kwa nyakati tofauti na  Mtandao huu  ,akiwemo Diwani wa viti Maalum tarafa ya Sengerema, Maswa Julieth Mongo wamesema hali ya soko ya zao la pamba inaridhisha ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo bei ya zao hilo ni Tsh.1400 hadi 1500 kwa kilo ikivuka lengo kwa bei elekezi ya serikali ambayo ni Tsh.1050.

Wamesema hali ya soko kwa mwaka huu imeleta matumaini makubwa kwao baada ya kukata tamaa kutokana soko ya bei ya zao la pamba kudodorora kwa muda mrefu lakini hali ya soko ya mwaka huu itahamasisha wakulima wengi kujikita katika zao hilo huku pia bei ya mwaka huu ni ya kupewa fedha taslimu ikilinganishwa na kipindi cha nyuma walikuwa wanakopwa pamba mpaka inapita miezi 6 ndipo wanalipwa.

Afisa Kilimo halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Gimu Yohana   Mabula amesema Wilaya hiyo imedhamiria kufikisha uzalishaji wa tani  laki moja na elfu thelathini[130,000 ]za zao la pamba katika msimu wa 2021/2022 ,lengo ni kuongeza uchumi wa Taifa katika utekelezaji wa kampeni ya uongezaji thamani zao la Pamba nchi nzima ambapo matarajio ni uzalishaji wa tani  za pamba milioni moja kote nchini.

Aidha,Afisa kilimo Mabula ameainisha upandaji  wa vipimo vipya vya zao la pamba kwa msimu wa 2021/22  ni  sentimita 60 kati ya mstari na mstari  na sentimita 30 kati ya shimo na shimo huku akisisitiza kuwa ifikapo Septemba 15,2021 kila mkulima  anatakiwa kuhakikisha masalia yote ya pamba shambani yawe yameshang’olewa na kuchomwa moto

Hata hivyo tunatarajiwa hivi karibuni kutembelewa na balozi wa Pamba Tanzania Agrey Mwanri  anatarajia kufika Wilayani Maswa  mkoani Simiyu  kuhamasisha kilimo cha pamba  .

Ikumbukwe kuwa mkoa wa Simiyu  umedhamiria kuongeza tija  uzalishaji zao la pamba kutoka  kilogram 200 kwa ekari  hadi kilogram 800  mpaka 1000 kwa ekari kwa msimu ujao 2021/2022  lengo ni uzalishaji wa tani laki tano

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »