Rais Samia Siluhu Hassan anashiriki Mkutano wa 41 wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC nchini Malawi.

Rais Samia Siluhu Hassan anashiriki Mkutano wa 41 wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC nchini Malawi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anashiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika leo tarehe 17 – 18 Agosti,2021 mjini Lilongwe nchini Malawi . Rais Samia Siluhu hassani aliwasili jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anashiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika leo tarehe 17 – 18 Agosti,2021 mjini Lilongwe nchini Malawi .

Rais Samia Siluhu hassani aliwasili jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu na kupokelewa na Mhe. Patricia Kaliati, Waziri wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii wa Malawi.

Katika Mkutano huo wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, Jamhuri ya Malawi itathibitishwa kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja (Agosti 2021 – Agosti 2022)

Aidha, Wakuu hao wa Nchi na Serikali watamthibitisha Katibu Mtendaji mpya wa SADC baada ya Katibu Mtendaji aliyepo Dkt. Stergomena Tax kumaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa ufanisi nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka nane.

Wakuu hao wa Nchi na Serikali wa SADC pia wanatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ya Mtangamano pamoja na kuidhinisha kauli mbiu  ya Jumuiya hiyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »