MCHUNGAJI AHUKUMIWA JELA MIEZI 6 KUTOANDIKISHA WATOTO SHULE

MCHUNGAJI AHUKUMIWA JELA MIEZI 6 KUTOANDIKISHA WATOTO SHULE

NA NYEMO MALECELA – KAGERA Mchungaji Merchedes Mugishagwe Buberwa (45) ambaye ni mkazi wa mtaa wa Kasarani ulioko Kata ya Bakoba Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela na faini ya shilingi milioni moja kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia kwa makosa matatu ya kwanza chini ya sheria ya

NA NYEMO MALECELA – KAGERA

Mchungaji Merchedes Mugishagwe Buberwa (45) ambaye ni mkazi wa mtaa wa Kasarani ulioko Kata ya Bakoba Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela na faini ya shilingi milioni moja kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia kwa makosa matatu ya kwanza chini ya sheria ya mtoto kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kama wazazi kwa madai kwamba kwenda shule kupata elimu ni kinyume na imani ya dhehebu lake la dini.

Kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2021 imetolewa hukumu jana (Ijumaa) na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, Daniel Nyamkelya.

Wakili wa serikali mkoani Kagera, Agrey Uhagile amesema mchungaji huyo na mkewe Agripina Maganja walikuwa wanakabiliwa na makosa nane lakini mahakama hiyo imewatia hatiani kwa makosa matatu ya kwanza chini ya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao kama wazazi.

Mchungaji huyo na mke wake walikamatwa na Polisi kwa amri ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kuhakikisha watoto hao wanaanza shule na kupangiwa madarasa kulingana na umri waliokuwa wao.

Watoto hao walianza masomo yao katika  shule ya msingi Buyekera ambapo Anna Merchedes (5) aliandikishwa darasa la awali, Joseline Merchedes (13) aliandikishwa darasa la nne na Joshua Merchedes (9) aliandikishwa darasa la pili.

Ili kulinda usalama wa wanafunzi hao kwa kuwa walikuwa mashahidi muhimu katika kesi hiyo, serikali iliamua kuwahamisha kutoka shule msingi ya Buyekela na kuwapeleka katika shule nyingine ya Bweni (jina limehifadhiwa) iliyopo katika Manispaa ya Bukoba.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »