CCM YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA DUWASA KUWASOGEZEA WANANCHI HUDUMA YA MAJI DODOMA

CCM YARIDHISHWA  NA UTENDAJI WA DUWASA KUWASOGEZEA WANANCHI HUDUMA YA MAJI DODOMA

Na Barnabas Kisengi Dodoma Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM unaofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) ya kuwasogezea wananchi huduma ya maji.Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Dodoma, Meja

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM unaofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) ya kuwasogezea wananchi huduma ya maji.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Dodoma, Meja Mstaafu Johnick Risasi wakati alipoongoza kamati ya siasa wilaya ya Dodoma Mjini kutembelea kituo cha kuzalisha Maji Mzakwe jijini Dodoma.

Meja Mstaafu. Risasi kuwa baada ya kamati ya siasa kutembelea na kukagua kazi inayofanywa na DUWASA imeridhika. “Kamati ya Siasa ya Wilaya imepita kukagua kazi inayofanywa na DUWASA na imejiridhisha na utekelezaji wa miradi ya Maji inayotekelezwa wilayani Dodoma. Nichukue nafasi hii kuwapongeza sana DUWASA kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi” alisema Meja Mst. Risasi kwa uhakika.


Akiongelea uhusiano baina ya upatikanaji wa huduma ya Maji na maendeleo, Mwenyekiti huyo alisema kuwa Maji yanachochea maendeleo. 
“Ndugu zangu Maji ni uhai, mnatuona tunatakata hapa kwasababu ya Maji. Tuwashukuru sana DUWASA kwa huduma hii nzuri. Bila Maji hatuwezi pata maendeleo. Mtakumbuka kuwa watu walikuwa wanatumia muda mrefu kutafuta huduma ya Maji. Sasa huduma hii inapofikishwa kwa wananchi, wanatumia muda zaidi katika shughuli za maendeleo” amesema Meja Mstaafu Risasi.


Akitoa maelezo ya hali ya huduma ya maji mjini Dodoma, Afisa mahusiano na Mawasiliano wa Duwasa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Sebastian Warioba ameseema kuwa hali ya uzalishaji na usambazaji wa maji ni nzuri. 
“DUWASA imefanikiwa kuunganisha huduma ya majisafi na salama kwa wateja 56,266 kupitia maunganisho haya, DUWASA imeweza kuhudumia wateja asilimia 62.7 ya wakazi” amesema Warioba.

Warioba amesema kuwa DUWASA imefanikiwa kuondoa mgao mkali wa maji uliokuwepo kabla ya kuanzishwa kwa DUWASA mwaka 1998. “DUWASA imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha huduma ya maji ikiwepo mradi ulioongeza uwezo wa uzalishaji maji Mzakwe.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »