RC SHIGELA AWATAKA WANCHI KUTUNZA MIRADI YA ISLAMIC FOUNDATION

RC SHIGELA AWATAKA WANCHI KUTUNZA MIRADI YA ISLAMIC FOUNDATION

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewataka wananchi Mkoani humo kutunza na kusimamia vizuri miradi yote inayotekelezwa na Taasisi ya The Islamic Foundation ili kujenga ustawi imara wa jamii ya watanzania. Shigela alitoa wito huo jana alipotembelea miradi mbalimbali inayotoa huduma za kijamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewataka wananchi Mkoani humo kutunza na kusimamia vizuri miradi yote inayotekelezwa na Taasisi ya The Islamic Foundation ili kujenga ustawi imara wa jamii ya watanzania.

Shigela alitoa wito huo jana alipotembelea miradi mbalimbali inayotoa huduma za kijamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na taasisi  hiyo.

Alisema wananchi wa Mkoa huo wanatakiwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi hiyo bila malipo yoyote na kuisimamia ipasavyo kwa manufaa ya watanzania kwa jumla.

“Natoa pongezi kubwa kwa Mwenyekiti wa The Islamic Foundation, ndugu yangu Aref Nahdi kwa maono chanya aliyonayo kwa wananchi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla, miradi hii inawajenga kiimani na kiroho katika kuachana na matukio ya kihalifu” amesema Shigela.

Rc Shigela alitembelea miradi mitano inayosimamiwa na taasisi hiyo ikiwemo Shule ya Sekondari ya Forest, Kituo cha Afya cha  Msamvu, Ujenzi wa bomba la maji Shule ya Msingi Msamvu A, Kituo cha watoto yatima na ujenzi wa Msikiti utakaoghalimu zaidi ya Shilingi Bil. 5 za kitanzania,

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TIF Aref Nahdi alimpongeza Shigela kwa kuitikia wito wa kutembelea miradi hiyo na kumuahidi kuendelea kujenga miradi mingine ya kijamii katika Mkoa wa Morogoro ikiwemo kutoa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Msing Msamvu A.

Alibainisha TIF ni taasisi ya kwanza Afrika kwa kufanya vizuri katika utoaji misaada katika jamii na ya tatu ulimwenguni kutokana na ukaribu wanaoujenga baina ya taasisi hiyo na viongozi wa Serikali.

Naye Victor Ngoyi, Mwakilishi kutoka MORUWASA ambao ni waufaika wa taasisi hiyo aliiomba TIF kuwafikishia maji wananchi sehemu ambazo hawajafika hususani maeneo ya pembezoni ili kuondoa kero ya upatikanaji wa maji wanayoipata wananchi.Attachments area

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »