CHADEMA: TUKO TAYARI KUZUNGUMZA NA RAIS SAMIA

CHADEMA: TUKO TAYARI KUZUNGUMZA NA RAIS SAMIA

Zifuatazo ni baadhi ya nukuu za Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tanzania Bara, Benson Kigaila alipozungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Oktoba 11, 2021 katika Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Mtaa wa Ufipa Kinondoni Jijini Dar es Salaam “Mwezi April Mwenyekiti Freeman Mbowe alimuandikia barua Rais Samia ya

Zifuatazo ni baadhi ya nukuu za Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tanzania Bara, Benson Kigaila alipozungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Oktoba 11, 2021 katika Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Mtaa wa Ufipa Kinondoni Jijini Dar es Salaam

“Mwezi April Mwenyekiti Freeman Mbowe alimuandikia barua Rais Samia ya kuhitaji kukutana naye, Rais Samia amekutana na makundi mbalimbali ila kundi la Wanasiasa bado, tuna imani ya kukutana naye tumweleze mambo yanayosababisha ufa kwenye Taifa hili”

“Nia na lengo letu la kuonana na Rais Samia sio kwenda kumueleza mambo yetu binafsi, bali mambo mbalimbali ya kuendesha Nchi yetu vizuri, na tuko tayari kwa mazungumzo na Rais, lakini hatuko tayari kukutana na Msajili”

“Baada ya kusikia kilio cha Wananchi kuhusu katiba mpya, tulimwandikia Rais Mstaafu Kikwete barua ya hitaji hilo akakubali kukutana nasi, tukashauriana na mchakato uliishia ulipoishia, alipoingia Rais Magufuli tuliandika barua nne na zote hazikujibiwa”

“Moja ya kazi kubwa ya chama cha siasa ni kuwasemea watu ambao hawana majukwaa ya kusemea mfano ni machinga na wengine, unapozuia mikutano ya vyama vya siasa maana yake umezua majukwaa ya Watu hao wasiseme na wasiwe na sauti za kusema”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »