PATO LA TAIFA LAONGEZEKA WA ASILIMIA 4.3

PATO LA TAIFA LAONGEZEKA WA ASILIMIA 4.3

Pato la Taifa la uchumi wa Taifa kwa  mwezi April –Juni, limeongezeka kwa kiwango cha asilimia 4.3, ikiwa ni pointi za asilimia 0.3 zaidi ikilinganishwa na ilivyokuwa katika robo ya pili ya mwaka 2020. Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa takwimu za uchumi, Daniel Masolwa, wakati akitoa taarifa ya ukuaji wa uchumi

Pato la Taifa la uchumi wa Taifa kwa  mwezi April –Juni, limeongezeka kwa kiwango cha asilimia 4.3, ikiwa ni pointi za asilimia 0.3 zaidi ikilinganishwa na ilivyokuwa katika robo ya pili ya mwaka 2020.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa takwimu za uchumi, Daniel Masolwa, wakati akitoa taarifa ya ukuaji wa uchumi wa robo ya pili kwa mwaka 2021.

Amesema pato la taifa kwa bei za miaka husika limeongezeka hadi shilingi trioni 39.2 kutoka tirioni 37.2 huku pato halisi la taifa likiongezeka hadi shilingi 33.4 kwa mwaka 2021 kutoka shilingi tirioni 32.0 mwaka 2020.

Ametaja chanzo cha ukuaji huo kuwa ni pamoja na shughuli za habari na mawasiliano kwa uzalishaji umeme, huduma nyingine za jamii zinazojumuisha sanaa na utamaduni, shughuli za kaya katika kuajiri,  malazi na huduma za chakula, usambazaji maji pamoja na uchimbaji madini na mawe.

Katika hatua nyingine Masolwa ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa za mikoa tajiri na maskini akidai kuwa uchambuzi wa takwimu hizo unahitaji weledi na kutumia viashiria zaidi vya pato la taifa, mfumuko wa bei, kiwango cha umaskini kiwango cha elimu, afya, maji, miundombinu ya usafiri na masoko ili kutoa taarifa sahihi kwa jamii.

katika robo ya pili ya mwaka 2021 ukuaji wa uchumi wa asilimia 4.3 umechangiwa na shughuli zote za uchumi,  zikihusisha kilimo kwa asilimia 13.0, uchukuzi na uhifadhi wa mizigo kwa asilimia 8.4, biashara na matengenezo asilimia 8.1, viwanda asimilia 7.6, madini asilimia 7.6, na ujenzi asilimia 7.1

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »