RAIS DK.MWINYI AMEFUNGUA IJITIMAI YA KIMATAIFA KIDOTI ZANZIBAR

RAIS DK.MWINYI AMEFUNGUA IJITIMAI YA KIMATAIFA KIDOTI ZANZIBAR

timai ya Kimataifa iliofanyika leo.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhadj Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa shukuran kwa waislamu wote waliochangia sadaka zao ili kufanikisha Ijitmai ya Kimataifa mwaka 2021 na kubainisha hatua hiyo kuwa ina fadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Alhadj Dk. Mwinyi amesema hayo katika hafla

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini alipowasili katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa 2021, inayofanyika leo 22-10-2021, katika Markaz hiyo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua maalum iliyosomwa na Amiri Lulu kutoka Gongolamboto Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi na Amiri Mkuu Ali Khamis Mwalim na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)

WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiitikia Dua ikisomwa na Amiri Lulu kutoka Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar, kabla ya ufunguzi wa Iji

timai ya Kimataifa iliofanyika leo.(Picha na Ikulu)

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa iliofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi, kufungua Ijitimai ya Kimatifa, inayofanyika katika Masjid FDiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikuu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Waumini wa Dini ya Kiislam katika hafla ya Ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 22-10-2021.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhadj Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa shukuran kwa waislamu wote waliochangia sadaka zao ili kufanikisha Ijitmai ya Kimataifa mwaka 2021 na kubainisha hatua hiyo kuwa ina fadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Alhadj Dk. Mwinyi amesema hayo katika hafla ya Ufunguzi wa Ijtimai ya Kimataifa inayoendelea kufanyika huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambapo imehudhuriwa na waislamu kutoka nchi mbali mbali za Ukanda wa Afrika Mashariki.

Akinukuu baadhi ya Aya za Qoraan Dk. Alhadj Mwinyi amesema Mwenyezi Mungu amewaahidi wanaotoa katika neema walizoruzukiwa watapa fadhila nyingi, hivyo akawasisitiza waislamu kuendeleza mwenendo mwema wa kupenda kukimbilia kutoa miongoni mwa neema walizonazo ili kufanikisha mambo ya kheri.Aliwataka kutumia fursa kama hiyo ya Ijtimai pamoja na mihadhara kwa ajili ya kukumbushana kwa kigezo cha kuwepo walinganiaji wanaoamrisha mema na kukataza maovu.

Dk. Alhadj Mwinyi aliwataka Masheikh watakaotoa mihadahara katika Ijtimai hiyo kuelezea changamoto za kuwepo vitendo vya udhalilishaji wa watoto na ukatili dhidi ya wanawake katika jamii na kusema vite ndo hivyo vinaitia aibu jamii kwa vile vinakwenda kinyume na mafundisho ya dini.“Ni wajibu wetu kila mmoja kutoa ushirikiano kwa Vyombo vya sheria, ili watoto wetu, kina mama na jamii yote kwa ujumla iweze kuondokana na janga la Udhalilishaji”, alisema.

Alisema jamii ina wajibu wa kuwalinda watoto kwa kuwapatia elimu na maadili mema ili waweze kukua wakiwa na maarifa na wacha Mungu.

Vile vile aliwataka waislamu na wananchi kote nchini kuendelea kuchukua tahadhari katika kukabiliana na Ugonjwa wa Corona au Uviko 19 kwa kuvaa Barakoa, kutumia vitakasa mikono kila mara pamoja na kupata chanjo ambazo kwa hakika ziko salama na hazina madhara yoyote kwani zmefanyiwa utafiti wa kutosha.Aidha, akatumia fursa hiyo kuhimiza umuhimu wa kudumisha amani , umoja na mshikamano, ikiwa ni hatua ya kupata maendeleo na mafanikio nchini.

Alhadj Mwinyi alitoa shukuran za dhati kwa Jumuiya ya Fiysabilillah Markazi kwa mafanikio makubwa iliopata katika utekelezaji wa malengo yake tangu ilipoasisiwa mwaka 1999, ikiwemo ujenzi wa Mskiti mkubwa wa Ijumaa uliojengwa ndani ya Markazi hiyo.Nae, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume alisema mahala hapo (markaz) ni chimbuko la umoja na akawakumbusha waislamu waliohudhuria Ijtmai hiyo umuhimu wa kuhesabiwa wakati utakapofika, jambo alilosema ni sehemu katika Dini ya Kiislamu.Aidha aliwataka masheikh watakaopata fursa ya kuendesha mihadhara katika Ijtmai hiyo kuzungumzia kw akina suala la Maadili katika jamii.Mapema, Mratibu wa Ijtmai hiyo Amir Wakati Hassan aliwaomba waislamu waliokusanyika kuzingatia mambo muhimu yatakayounganisha umma wa kiislamu badala ya kuwatenganisha, ikiwa ni pamoja na kuepuka siasa na hitilafu mbali mbali ziliomo katika madhehebu ya waumini.

Ijtimai ya Kimataifa ya 2021, imeandaliwa na Jumuiya ya Fyisabilillah Tabligh Markaz, ikiwa inafanyika katika Mskiti mkubwa wa Ijumaa uliomo ndani ya Markaz hiyo, ambao unakadiriwa kuwa na uwezo wa kuswaliwa na waumini wapatao 5,500 kwa wakati mmoja.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »