Rais Dkt. Mwinyi amefungua na kuweka jiwe la msingi nyumba za makazi ya kukodisha na hoteli kubwa.

Rais Dkt. Mwinyi amefungua na kuweka jiwe la msingi nyumba za makazi ya kukodisha na hoteli kubwa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. HusseinAli Mwinyi amesema Serikali inavutia Wawekezaji wa aina zote kujakuwekeza katika miradi mbali mbali nchini, ili kusaidiana kukuzauchumi.Dk. Mwinyi amesema hayo katika ufunguzi na uwekaji wa jiwe lamsingi wa nyumba za maakazi ya kukodisha (apartments), haflailiofanyika Bweleo na Mbweni Jijini Zanzibar.Katika hafla hiyo Rais Dk.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi amesema Serikali inavutia Wawekezaji wa aina zote kuja
kuwekeza katika miradi mbali mbali nchini, ili kusaidiana kukuza
uchumi.
Dk. Mwinyi amesema hayo katika ufunguzi na uwekaji wa jiwe la
msingi wa nyumba za maakazi ya kukodisha (apartments), hafla
iliofanyika Bweleo na Mbweni Jijini Zanzibar.
Katika hafla hiyo Rais Dk. Mwinyi aliweka jiwe la msingi Nyumba za
makaazi ya kukodisha ya ‘Blue Ocean Residents’ iliopo Bweleo
pamoja na Al- Saadi ilioko Mbweni.
Amesema kupitia miradi ya aina hiyo, wananchi wengi watapata fursa
ya kufanya kazi sambamba na Serikali kukusanya kodi, hivyo
kuiwezesha kukuza uchumi wake.
Alisema wakati umefika wa Serikali kuanzisha miji mipya baada ya ile
ya zamani, ikiwemo Kilimani majengo yake kuchakaa kabisa na
kubainisha kazi hiyo umuhimu wa sekta binfasi kuiunga mkono
Serikali katika kufanikisha azma hiyo.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwapongeza Wawekezaji wa majengo hayo
kwa kuja na miradi hiyo yenye lengo la kuvutia Wawekezaji kupata
nyumba za kuwaweka wafanyakazi wao wakati wakitekeleza miradi
yao hapa nchini.
Nao, wawekezaji wa miradi hiyo wameahidi kutoa kipaumbele cha
nafasi za ajira kwa vijana wa Zanzibar pamoja na kutoa fursa za
mafunzo ya Hoteli ili waweze kunufaika kwa kuwepo miradi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar
(ZIPA) Sharrif Ali Shariff alisema mamlaka itaendelea kushirikiana na

wawekezaji ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao.
Kitengo cha habari,
Ikulu Zanzibar

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »