Kamati ya Ukaguzi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) imekumbushwa kufuata sheria na miongozo.

Kamati ya Ukaguzi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) imekumbushwa kufuata sheria na miongozo.

Wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wamekumbushwa kufuata sheria, taratibu na miongozo inayotolewa ya kamati hiyo ili kuboresha ufanisi wa kazi na kutimiza malengo ya Chuo. Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda  wakati akifungua mafunzo ya Siku mbili kwa Kamati

Wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wamekumbushwa kufuata sheria, taratibu na miongozo inayotolewa ya kamati hiyo ili kuboresha ufanisi wa kazi na kutimiza malengo ya Chuo.


Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda  wakati akifungua mafunzo ya Siku mbili kwa Kamati ya Ukaguzi wa ndani ya Chuo iliyofanyika ukumbi wa Kituo cha Kuratibu Hewa ya Ukaa katika Kampasi ya Edward Moringe Morogoro.


“Mimi nina matumaini makubwa sisi sote tunaoshiriki mafunzo haya tutakuwa wasikivu na tutajipa muda ili kuelewa na kukubali kukumbushwa majukumu na umuhimu wa shughuli za ukaguzi katika kusimamia majukumu ya Chuo” ,amesema Prof. Chibunda.


Prof. Chibunda amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Kamati ya Ukaguzi ya mwaka wa fedha 2021/2022 na ni sehemu ya kutekeleza Hati Idhini ya Kamati kuwa yatolewe mafunzo mafupi kwa wanakamati wa kamati ya ukaguzi.


“Kama wengi wetu tunavyofahamu Kamati hii ndio jicho la Baraza katika usimamizi kuhakikisha kwamba utendaji wetu unazingatia kanuni, taratibu, sera, mifumo na miongozo mbalimbali ya kiserikali na ile ambayo inatolewa na Baraza letu la Chuo”, amesema Prof. Chibunda.


Pia ameelezea dhumuni la mafunzo hayo kuwa ni kuwaongezea uelewa kamati ya ukaguzi na kuwakumbusha majukumu yao na umuhimu wa kamati ya ukaguzi katika kushauri Baraza la Chuo kwenye utekelezaji wa majukumu yao hususani katika usimamizi wa chuo.


Aidha ameongezea kuwa mafunzo hayo yalihusisha pia Menejimenti ya Chuo kutokana na Kamati ya Ukaguzi kufanya kazi karibu na Menejimenti hiyo hivyo mafunzo hayo yatawasaidia wote kuelewa pamoja  masuala muhimu ya Usimamizi wa Rasilimali za Chuo na kujiandaa na viatarishi mbalimbali vinavyokikabili Chuo hicho.


Naye mtoa mada katika mafunzo hayo ambaye ni Muasisi wa  Taasisi ya Ukaguzi wa ndani (TIA) Godfrey Kilenga ameshukuru kwa mualiko alioupata kutoka SUA kutoa mafunzo hayo na kwamba ana Imani yataleta mabadiliko makubwa Chuoni hapo.


Amesema kuwa miongozo mingi ya shughuli za ukaguzi inatoka serikalini hivyo ni vizuri  wajumbe hao kufanyia kazi yatakayofundishwa ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutimiza malengo waliyojiwekea.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »