MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA BONAH AMPONGEZA RAIS SAMIA

MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA BONAH AMPONGEZA RAIS SAMIA

NA HERI SHAABAN MBUNGE wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Hassan Suluhu,kwa kuipatia jimbo la Segerea Bilioni 1.6 kwa ajili ya madarasa ya UVIKO 19. Mbunge Bonah alitoa pongeza hizo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakati wa ziara yake ya Sekta ya Elimu kukagua madarasa

NA HERI SHAABAN

MBUNGE wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Hassan Suluhu,kwa kuipatia jimbo la Segerea Bilioni 1.6 kwa ajili ya madarasa ya UVIKO 19.

Mbunge Bonah alitoa pongeza hizo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakati wa ziara yake ya Sekta ya Elimu kukagua madarasa ya elimu sekondari.

“Nampongeza Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani jimbo langu la Segerea nimepewa shilingi Bilioni 1,620,000,000 kwa ajili ya msdarasa ya UVIKO wanafunzi wetu waje kusoma ” alisema Bonah

Mbunge Bonah alisema Taifa lolote ili liweze kuendelea lazima watu wake wasome atasimamia madarasa hayo kila kata na madiwani wa kata zote kuakikisha madarasa yanaisha kwa wakati.

Katika ziara hiyo Mbunge Bonah alitembelea Kata ya Kinyelezi ,Kimanga na Bonyokwa katika kata ya Kinyelezi mbunge Bonah alitoa ahadi ya Fedha za Mfuko wa Jimbo kujenga vyoo vya Walimu sekondari ya kinyelezi mpya yenye changamoto ya vyoo .

Diwani wa Kinyelezi Leah Ngitu alisema kata ya kinyelezi wamepewa milioni 200 kwa ajili ya kituo cha afya cha kata hiyo .

Leah alimpongeza Mbunge Bonah kutatua changamoto za kata hiyo kwa fedha za Mfuko wa jimbo .

Diwani wa Bonyokwa Tumike Malilo alimpongeza Mbunge kwa kuwavutia umeme sekondari ya Bonyokwa ambapo kwa sasa wanafunzi wanasoma katika mangira bora na salama .

Diwani tumike alisema mikakati yake Kata ya Boyokwa wanafunzi wasome kidato cha tano na kidato cha sita ambapo alimshauri mbunge ili kurahisisha wanafunzi shule za kata wasome karibu

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »