Dodoma Baadhi ya Wananchi kutoka maeneo mbalimbali mkoani Dodoma wamesema mwaka 2021 umekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupanda kwa bei za bidhaa hali ambayo imesababisha ukali wa maisha huku wakisema hawatausahau mwaka huo kutokana na kuondokewa na kiongozi mkubwa wa nchi,Hayati John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania huku wakielezea matumaini yao ya kuupokea mwaka
Dodoma
Baadhi ya Wananchi kutoka maeneo mbalimbali mkoani Dodoma wamesema mwaka 2021 umekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupanda kwa bei za bidhaa hali ambayo imesababisha ukali wa maisha huku wakisema hawatausahau mwaka huo kutokana na kuondokewa na kiongozi mkubwa wa nchi,Hayati John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania huku wakielezea matumaini yao ya kuupokea mwaka mpya 2022 .
Wakizungumza na Kituo hiki kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao wamesema mambo mengi yametokea mwaka 2021 yakiwemo mazuri pamoja na changamoto hivyo mwaka mpya 2022 ni mwaka wa kujitafakari na kujisahihisha katika kukabiliana na changamoto za maisha huku wakisema hawatausahau mwaka 2021 kwa kumpoteza Hayati John Pombe Magufuli.
Nao baadhi ya Viongozi wa dini akiwemo Mkuu wa Idara ya vijana baraza kuu la Waislam Tanzania [BAKWATA] Sheikh Omary Salim ambaye pia ni sheikh wa msikiti wa Dar Mustapha Chang’ombe Dodoma pamoja na kiongozi wa kanisa la Baptist Tanzania ,Makole Dodoma Mchungaji Anthony Mlyashimba wakatoa wakampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya huku wakitoa ushauri kwa mwaka mpya 2022.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *