Mhe. Soraga amesema Serikali ya Zanzibar inahitaji sana kukamilisha mradi wa hospitali ya Binguni ili kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Mhe.  Soraga amesema Serikali ya Zanzibar inahitaji sana kukamilisha mradi wa hospitali ya Binguni ili kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais – Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inahitaji sana kukamilika kwa mradi wa hospitali ya Binguni ili kutoa huduma bora na nafuu kwa Wananchi Ameyasmea hay oleo ofisini kwakwe mwanakwerekwe mjini unguja wakati akizungumza na wawekezaji wa kutoka kampuni ya MAZI

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais – Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inahitaji sana kukamilika kwa mradi wa hospitali ya Binguni ili kutoa huduma bora na nafuu kwa Wananchi

Ameyasmea hay oleo ofisini kwakwe mwanakwerekwe mjini unguja wakati akizungumza na wawekezaji wa kutoka kampuni ya MAZI Concessions walioonyesha nnia ya kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo ya binguni iliyopo ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja.

Waziri Soraga amesema ujenzi wa Hospitali hiyo una lengo la kutoa huduma kwa wananchi wa hali ya chini hivyo ipo haja baina ya serikali na wadau hao  kukaa pamoja na kuona ni kwa jinsi gani hospitli hiyo itatoa huduma nafuu kwa wananchi pamoja na wawekezaji hao kunufaika na uendeshaji wa Hospitali hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu anaeshighulikia masuala ya Uchumi na Uwekezaji Dk Habiba Hassan Khamis amesema kumekuwa na maombi mengi kutoka kwa wadau mbali mbali kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo lakini changamoto kubwa ni kuafikiana katika suala zima la kurudisha grama za ujenzi na  uedeshaji wa hospitali hiyo na kuweza kupata faida kwa wawekezaji wa sekta binafsi

Aidha Dk Amour Suleimn Mohd Mkurugenzi Tiba  Hospitali ya Mnazi mmoja Amesema lengo la ujenzi ya hospitali ya binguni ni kuwa na hospitali ambayo itatoa mafunzo ya udaktari kwa watu mbali mbali wa ndani na nje ya nchi ambapo itakuwa kambi maalumu ya kuweza kuhudumia na kupunguza garama kwa wagonjwa ambao watahitaji matibu nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya MAZI Concessions Sisye Elon Henry amesema hospitali hiyo itasimamia na sekta binafsi licha ya kuwa itakuwa chini ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na lengo lake ni kuona mashirikiano baina ya sekta binasfi na Serikali yanapelekea utoaji wa huduma bora za hospitali zenye hadhi ya Kimataifa kwa Wananchi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »