Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa kutumia misikiti kwa kujenga jamii bora na isiwe tu kwa kufanya Ibada .

Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa kutumia misikiti kwa kujenga jamii bora na isiwe tu kwa kufanya Ibada .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo alipojumuika na waumini wa Masjid Twayyib uliopo Fuoni kituo cha polisi Wilaya ya Magharibi “B” unguja katika Ibada ya Sala ya Ijumaa. Amesema jamii tulionayo inahitaji malezi zaidi hasa ya kumjua mola wao ambapo kwa kufanikiwa katika suala hilo kutaweza kusaidia zaidi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo alipojumuika na waumini wa Masjid Twayyib uliopo Fuoni kituo cha polisi Wilaya ya Magharibi “B” unguja katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema jamii tulionayo inahitaji malezi zaidi hasa ya kumjua mola wao ambapo kwa kufanikiwa katika suala hilo kutaweza kusaidia zaidi kupunguza matendo maovu katika jamii, kama vile ya ubakaji, madawa ya kulevya pamoja na udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

Amesema umefika wakati wa kurudi katika mila, silka na tamaduni za kizanzibari za kulea kwa pamoja  na kukemea tabia ya wizi hasa katika sehemu za Ibada na kueleza kuwa asilimia kubwa ya wanaofanya matendo hayo wameathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Mhe. Hemed  amesema Serikali inategemea nguvu kazi ya vijana katika kuleta maendeleo hasa kutumika katika kujenga miradi ya mbali mbali ya maendeleo ambayo Serikali ya Awamu ya Nane imeipanga katika kuwaletea huduma bora za kijamii wananchi wake

Mhe. Hemed ameitaka Jamii kuendelea kuwa wamoja hasa panapotokea hitilafu za kukosana kibinadamu kwa kushirikiana na kuondoa tofauti hizo, ili kuweza kupata jamii yenye umoja na mshikamano baina yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia  watu wenye mahitaji maalum wakiwemo watu wenye ulemavu, Mayatima, wajane na Maskini ili kuendeleza utamaduni uliokuwepo miaka iliyopita katika visiwa vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Akitoa Khutba Mskitini hapo Ustadh Mahmoud Abeid Hamid amewakumbusha  waumini wa Dini ya Kiislamu kuacha tabia ya kudhulumu nafsi zao kwa kisingizio cha maisha kuwa magumu ,na kuamini kuwa Allah ndie mtoaji wa Riski.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »