Kifo cha Kigogo huyu chamshtua Rais Samia

Kifo cha Kigogo huyu chamshtua Rais Samia

Mwenyekiti wa Chama  cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema chama kimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mwanasiasa mkongwe  nchini,  John Nchimbi kilichotokea Jumapili 23 Januari, 2022. Nchimbi amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika  Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam. Samia amemtaja marehemu  Nchimbi kuwa enzi

Mwenyekiti wa Chama  cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema chama kimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mwanasiasa mkongwe  nchini,  John Nchimbi kilichotokea Jumapili 23 Januari, 2022.

Nchimbi amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika  Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.

Samia amemtaja marehemu  Nchimbi kuwa enzi ya uhai wake akiwa kada TANU na baadaye CCM, alikuwa mstari wa mbele  kukitumikia chama.

Rais Samia amesema Nchimbi alikuwa mwanachama shupavu aliyetumia muda na maisha yake yote  kukitumikia chama na Taifa  kwa uaminifu na uzalendo mkubwa.

“Siku chache zijazo  CCM kitatimiza miaka 45 tangu kizaliwe, Nchkmbi amekuwa na mchango mkubwa, tutamkumbuka  kwa uongozi wake uliotukuka,  ujasiri, utiifu na aliyekitumikia chama  kwa uadilifu na mapenzi makubwa.  Hakuwa mtu anayekata tamaa hasa katika kufanikisha masuala muhimu yanayogusa maslahi mapana ya chama na Taifa,” amesema Samia.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema enzi ya uhai wake,  Nchimbi amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM na miongoni mwazo ni pamoja na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa  (NEC) na Katibu wa CCM wa mikoa ya Kigoma, Singida na Dar es Salaam kwa nyakati tofauti na aliwahi kuwa mkufunzi wa vyuo vya chama vya Ilonga na Kivukoni.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »