MAJALIWA: VIJANA JIWEKEENI MALENGO YA KULISAIDIA TAIFA

MAJALIWA: VIJANA JIWEKEENI MALENGO YA KULISAIDIA TAIFA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wa Kitanzania wahakikishe wanajiwekea malengo ya kusoma kwa bidii ili kupata maarifa yatakayolisaidia Taifa kupata maendeleo. Pia, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Januari 24, 2022)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wa Kitanzania wahakikishe wanajiwekea malengo ya kusoma kwa bidii ili kupata maarifa yatakayolisaidia Taifa kupata maendeleo.

Pia, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Januari 24, 2022) alipokagua ujenzi wa madarasa ya shule za Sekondari za Gehandu na Nowu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali kwa upande wake imejipanga ipasavyo na itaendelea kuweka mazingira bora ya kujifunza na kufundishia ili kuwawezesha kufikia malengo yao.

Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19. “Vijana someni kwa bidii hadi mfike chuo kikuu.”

Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote ziweke mpango wa ujenzi wa mabweni kupitia mapato yao ya ndani ili wanafunzi wakae shuleni na kupata muda wa kutosha wa kujisomea.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi wa umma kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuwatumikia Watanzania na kutekeleza maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya CCM.

Awali, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Gehandu, Mwalimu Gadiel Bei alimshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa.

Alisema mbali na madarasa hayo pia wamejenga madarasa mengine matano kati yake mawili yametokana na fedha za ruzuku ya EP4R na matatu ni nguvu za wananchi na Halmashauri.

Mwalimu Bei alisema kukamilika kwa madarasa hayo kutaiwezesha shule hiyo yenye wanafunzi 945 wa kidato cha kwanza hadi cha sita kuongeza tahasusi nyingine ya kidato cha tano kuanzia mwezi Julai 2022.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »