Tanzania na Uturuki kushirikiana katika Sekta ya Utamaduni

Tanzania na Uturuki kushirikiana katika Sekta ya Utamaduni

Na Shamimu Nyaki – WUSM, Dodoma Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Saidi Yakubu amekutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu  kuhusu kushirikiana katika Sekta ya Utamaduni nchini. Kikao hicho cha kupitia Mkataba wa Ushirikiano  katika Sekta za Wizara kabla ya kuusaini  kiilifanyika Mei 10, 2022

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Saidi Yakubu
akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu
na watendaji wengine wa wizara baada ya kikao kuhusu kushirikiana katika Sekta ya
Utamaduni nchini, kilichofanyika Mei 10, 2022 Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Saidi Yakubu
akizungumza katika kikao na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu na
watendaji wengine wa wizara baada ya kikao kuhusu kushirikiana katika Sekta ya
Utamaduni nchini, kilichofanyika Mei 10, 2022 Dodoma.
Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu akizungumza katika kikao
kuhusu nchi yake kushirikiana na Tanzania katika Sekta ya Utamaduni kilichofanyika
Mei 10, 2022 Dodoma.

Na Shamimu Nyaki – WUSM, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Saidi Yakubu amekutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu  kuhusu kushirikiana katika Sekta ya Utamaduni nchini.

Kikao hicho cha kupitia Mkataba wa Ushirikiano  katika Sekta za Wizara kabla ya kuusaini  kiilifanyika Mei 10, 2022 Dodoma ambapo Naibu Katibu Mkuu Yakubu, ameeleza kuwa Tanzania na  Uturuki ni marafiki ambao wamekua wakibadisilishana  Utamaduni wa nchi hizo ikiwemo tamthiliya na filamu mbalimbali.

“Nchi yetu ni marafiki Wazuri wa nchi yenu, wananchi wanaangalia tamhiliya za nchini kwenu na wanazipenda, Hivyo urafiki wetu utasaidia nchi yetu kutangaza Utamaduni wake katika nchi yenu ya Uturuki” Alisema Bw. Yakubu.

Bw.Yakubu amemtumia nafasi hiyo kumuomba Mhe Balozi  Mehmet kulitumia Baraza la Kiswahili nchini (BAKITA) kwa ajili ya kupata wataalamu, vitabu vya kujifunza lugha ya Kiswahili  kwa ajili ya Taasisi za elimu za nchi hiyo  ambazo zina nia ya kufundisha waturuki  lugha  ya kiswahili  ambayo ni miongoni mwa lugha zenye wazungumzaji wengi duniani.

Aidha, Bw.Yakubu ameikaribisha Uturuki kushiriki katika Tamasha kubwa la Utamaduni na Sanaaa la Bagamoyo linalotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu ili iweze kuonyesha Utamaduni wao.

Kwa upande wake Mhe.Balozi ameeleza Nia ya Nchi yake kuanzisha Kituo cha Utamaduni jijini Dar es Salaam ambacho kina lengo la kuonyesha kazi mbalimbali za Kitamaduni za nchi hiyo ambazo zitatoa fursa kwa Watanzania kujifunza mambo mbalimbali ya nchi hiyo na kuongeza fursa ya kuingia katika soko la nje. 

“Tunaishukuru Tanzania kwa urafiki mzuri, na ushirikiano uliopo baina yetu katika Sekta mbalimbali, na Sasa tunaenda kushirikiana katika Utamaduni kwetu sisi ni jambo kubwa na tunaamini litaleta tija kwa nchi zote mbili.

Mhe.Balozi ameongeza kuwa Uturuki itaendelea kushirikiana na Wizara katika Sekta nyingine za Sanaa na Michezo.

Kikao hicho  kimehudhuriwa pia na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu na Wakurugenzi wengine wa wizara hiyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »