Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yapanua wigo kwa wabunifu kutenga bilioni 5.5

Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yapanua wigo kwa wabunifu kutenga bilioni 5.5

Na Barnabas Kisengi, Dodoma Wabunifu watengewa bilioni 5.5 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Eliamana Sedoyoka amesema Serikali imepanua    wigo wa bajeti ya masuala ya ubunifu nchini kutoka Sh.Bilioni moja kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia Sh.Bilioni 5.5 kwa mwaka ujao wa fedha 2022/23. Hayo yameelezwa leo  Jijini Dodoma  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Prof.Eliamani Sedoyeka,wakati

Na Barnabas Kisengi, Dodoma

Wabunifu watengewa bilioni 5.5

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Eliamana Sedoyoka amesema Serikali imepanua    wigo wa bajeti ya masuala ya ubunifu nchini kutoka Sh.Bilioni moja kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia Sh.Bilioni 5.5 kwa mwaka ujao wa fedha 2022/23.

Hayo yameelezwa leo  Jijini Dodoma  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Prof.Eliamani Sedoyeka,wakati akifungua   mafunzo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO.

Amesema  katika bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2021/22 ambao unaishia Juni 30, mwaka huu, kiasi cha Sh.Bilioni moja kilitengwa kwa ajili ya kuendeleza wabunifu.

Katibu huyo amesema fedha hizi zipo Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia (COSTECH)  na tayari wapo wabunifu ambao wamepokea na wanaendelea kupokea.

Prof. Sedoyeka,amesema   kwa mwaka ujao(2022/23), Serikali imepanga kutenga Sh.Bilioni 5.5 kwa ajili ya kuweka mazingira wezeshi ya kubuni na kuendeleza bunifu, kujengea uwezo taasisi na mbunifu mmoja mmoja.

“Mtu akifanya bunifu tunamshauri sana kwenda serikalini kulingana na ubunifu wake, lakini Shirika la Viwango Tanzania(TBS) kushauri viwango vinavyotakiwa kulingana na ubunifu uliobuniwa, pia bunifu zifanywe kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi, ”alisema.

Amesema hadi sasa wabunifu ambao wametambuliwa, kuziangalia teknolojia na kuziingiza kwenye vituo atamizi kwa matumizi ya nchi ni takribani 200 na Sh.Bilioni 2.3 zimetumika kuendeleza gunduzi zao.

Katibu Mkuu huyo amesema kati ya bunifu ambazo zimefanya vizuri sana ni Magila Tech alikoanzia  akiwa mwanafunzi IFM na kwenda COSTECH na  akapewa ushirikiano  na serikali.

“Sasa hivi yeye ni kati ya wabobezi duniani katika usalama wa mitandao, na juzi amefungua ofisi Dubai ikiwa ni Ofisi yenye vijana wa kitanzania saba, NIT pia wameshatengeneza gari, nimeona Kipanya ametengeneza gari, ukienda Arusha Tech imetengeneza gari ndogo kwa ajili ya wenye changamoto za kutembea kwa miguu, ambayo inatumia umeme jua,”alisema.

Naye,Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Maulilio Kipanyula amesema Mashindano ya mwaka huu yameshindanisha wabunifu 862 kutoka makundi ya shule ya Msingi na Sekkondari, Vyuo vya Ufundi, Vyuo vya Ufundi wa Kati, Mfumo usio rasmi, Taasisi za Utafiti na Vyuo Vikuu.
Amesema  kuwa Wizara imeendelea kuandaa mazingira wezeshi ili wabunifu waweze kuonekana pamoja na bunifu zao ziweze kufika sokoni, kushirikiana na wadau katika kutekeleza hilo na kutenga bajeti ili kuendeleza wabunifu.
Kwa upande wake Meneja wa Programu ya FUNGUO ya UNDP, Joseph Manirakiza amesema wamekuwa wakishirikiana na Wizara katika kuwaendeleza wabunifu, kutoa msaada wa kitaalamu kwa wabunifu hao kupitia kumbi za atamizi lakini pia kushirikiana na Serikali kuweka mazingira rafiki ya wabunifu katika kuendesha biashara.
Wiki ya Ubunifu Tanzania kwa mwaka huu ina kauli mbiu “Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu” na inashirikisha wabunifu 70 ambao wameshindanishwa kutoka kwa wabunifu 862 waliowasilisha bunifu zao.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Waandishi Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mwandishi wa Redio Uhuru,Sakina Abdulmasoud  ameishukuru Wizara hiyo kwa kuandaa semina ambayo imewasaidia kupata uelewa kuhusu mambo ya ubunifu.

Sakina ambaye ni Balozi wa Mazingira,amewataka wabunifu kubuni teknolojia ambazo ni rafiki katika masuala ya mazingira huku akidai  wataendelea kufanya kazi pamoja na Wizara hiyo huku akikipongeza kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara hiyo kwa kuonesha ushirikiano mkubwa kwa waandishi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »