BASHE AAGIZA BODI ASA KUTANGAZA ZABUNI YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI SHAMBA LA ARUSHA LA KUZALISHA MBEGU

BASHE AAGIZA BODI ASA KUTANGAZA ZABUNI YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI SHAMBA LA ARUSHA LA KUZALISHA MBEGU

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe leo Juni 5, 2022 ameiagiza Bodi ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kuanza  mchakato Kutafuta mzabuni atakayejenga mfumo thabiti wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika shamba la ASA lililopo Ngaramtoni jijini Arusha. Bashe ametoa agizo hilo wakati alipotembelea shamba hilo la uzalishaji wa mbegu za

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe leo Juni 5, 2022 ameiagiza Bodi ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kuanza  mchakato Kutafuta mzabuni atakayejenga mfumo thabiti wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika shamba la ASA lililopo Ngaramtoni jijini Arusha.


Bashe ametoa agizo hilo wakati alipotembelea shamba hilo la uzalishaji wa mbegu za arizeti, ngano na soya alilolikuta likiwa halina uzio na wala hakuna miundombinu ya umwagiliaji na huduma nyingine muhimu.


Bashe amesema mbali na kujengwa mfumo utakaosaidia kilimo cha umwagiliaji shamba hilo pia linatakiwa kusafishwa.
Pia Bashe amesema ili mashamba ya ASA kuendelea kuwa salama ni lazima yawe kwenye mfumo ambao unawazuia wananchi kuyavamia na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.


Amesisitiza kuwa ASA haitoweza kuzuia uvamizi wa wananchi kwenye mashamba yao kama wakishindwa kuyalinda ambapo alishauri kujengwa kwa nguzi za zege kisha kuunganishiwa senyenge kuzunguka mashamba yote ya ASA.
“Huwezi kumzuia mtu asivamie mashamba haya kama haujaweka uzio na tena mkubwa ambao unalenga kuimarisha usalama wa maeneo ya mashamba, hii itazuia hata wafugaji kuingiza ng’ombe kwenye mashamba yenu ya kuzalisha mbegu” alisema Bashe.


Pia Bashe amesema ikifika Julai mosi mwaka huu anataka kuona wakandarasi waliopewa zabuni za ujenzi wa miradi ya umwagiliaji wameshaanza kazi na kuwa atakuwa akipita kukagua miradi hiyo na kuitaka Tume ya Umwagiliaji kusimamia kuanza kwa kandarasi za ujenzi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »