Serikali itaendelea kuheshimu mchango wa madhehebu ya dini.

Serikali itaendelea kuheshimu mchango wa madhehebu ya dini.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuthamini, kutambua na kuheshimu mchango wa madhehebu ya dini katika kujenga mustakabali wa nchi yetu. Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Juni 26, 2022) katika ibada ya kusimikwa kwa Askofu Mteule Wolfgang Pisa, Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi katika viwanja vya Ilulu, Lindi. “Maendeleo ya nchi hayawezi kuimarika

May be an image of 4 people, people standing and indoor
May be an image of 3 people, people sitting, people standing and suit

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuthamini, kutambua na kuheshimu mchango wa madhehebu ya dini katika kujenga mustakabali wa nchi yetu.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Juni 26, 2022) katika ibada ya kusimikwa kwa Askofu Mteule Wolfgang Pisa, Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi katika viwanja vya Ilulu, Lindi.

“Maendeleo ya nchi hayawezi kuimarika kama tutakuwa wabinafsi. Tukiimarisha ushirikiano na ushirikishwaji wa kila mtu, tutaleta maendeleo ya Taifa letu kwa haraka.”

Amesema Serikali imeendelea kushirikiana na dini zote katika kukuza ustawi wa wananchi kiuchumi na kijamii ili kuimarisha maisha ya kila Mtanzania na Taifa kwa ujumla.

Amesema kwa kuzingatia hayo, Serikali imekuwa ikishirikiana na sekta binafsi zikiwemo taasisi za dini katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi na kuleta maendeleo ya Taifa.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inatambua na kuthamini kazi na majukumu makubwa ya viongozi wote wa dini.

Mheshimiwa Majaliwa amesema miongoni mwa majukumu hayo ni pamoja na kuwaongoza watu kiroho kwa kuwapa mafundisho, kutoa ushauri na kuwajenga kiimani.

“Vilevile, mmekuwa mkiwasaidia watu katika shida mbalimbali hususan wale wenye uhitaji kama yatima na wajane sambamba na kutoa ushauri nasaha na malezi bora kwa vijana.”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »