SERIKALI YATENGA BILIONI 263 KUBORESHA HOSPITALI YA RUFAA YA DODOMA

SERIKALI YATENGA BILIONI 263 KUBORESHA HOSPITALI YA RUFAA YA DODOMA

Na. Mwandishi wetu- Dodoma Serikali ilitoa Shilingi Bilioni 263 ya fedha za ahueni ya UVIKO-19 ili kuboresha Hospitali za rufaa za mikoa kati ya fedha hizo hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ilipewa kiasi cha bilioni 4.6 ambazo zimeweza kujenga jengo la wagonjwa mahututi litakalokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 50 kwa wakati mmoja

Na. Mwandishi wetu- Dodoma


Serikali ilitoa Shilingi Bilioni 263 ya fedha za ahueni ya UVIKO-19 ili kuboresha Hospitali za rufaa za mikoa kati ya fedha hizo hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ilipewa kiasi cha bilioni 4.6 ambazo zimeweza kujenga jengo la wagonjwa mahututi litakalokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 50 kwa wakati mmoja pamoja na ununuzi wa vifaa tiba.


Hayo yamebainiashwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Hospitali hiyo kujionea utekelezaji wa fedha hizo ambapo kunajengwa jengo la wagonjwa mahututio, jengo la Radiolojia (CT-Scan), nyumba ya mtumishi pamoja na ukarabati wa jengo la huduma za dharura (EMD).


Amesema kutokana na jengo la wagonjwa mahututi (ICU) linaendelea vizuri na hivyo litasaidia kuongezeka kwa vitanda vya wagonjwa mahututi hadi kufikia wagonjwa 50 kutoka wagonjwa 18 hapo awali.
“Fedha hizi tulizowezeshwa na Rais Samia Suluhu Hassan, sasa Wizara ya afya kipaumbele chetu ni ubora wa huduma, hivyo kutokana na vitanda hivyo tutaweza kuwahudumia wagonjwa 50 ikiwa ni  utekelezaji wa maono na dhamira ya Mheshimiwa Rais”. Amesema Waziri Ummy.


Aidha, Waziri Ummy amesema kwa jengo la Radiolojia ambalo litawekwa mashine ya CT-Scan ambapo huduma hiyo haikuweppo hapo awali na hivyo itaweza kupunguza mzigo kwa wakazi wa Dodoma ambao walikuwa wanaenda kupata vipimo hivyo kwenye hospitali ya Benjamini Mkapa.
“Hospitali hii kwa  mwezi wanapata wagonjwa 75 hadi 100 ambao wanapaswa kufanyiwa kipimo cha TC-Scan, hivyo huduma hii itawawezesha wananchi kupata kwa bei rahisi na kuwaondolea usumbufu hadi hospitali ya kanda ya Benjamini Mkapa”. Aliongeza Waziri Ummy.


Kwa upande wa ukarabati wa jengo la huduma la dharura (EMD) Waziri huyo amesema huduma zote za dharura zitapatikana  katika eneo moja hivyo Serikali imeweza kuboresha huduma za wagonjwa dharura kwani kutokuwa na huduma hizo unawezaa kupoteza maisha ya watu.


Hata hivyo Waziri Ummy amekiri kutokutosha kwa vitanda kwenye  huduma za dharura  kutokana na ongezeko la watu pamoja na ufinyu wa eneo la hospitali hiyo  kuahidi kufanya mazungumzo  jiji la Dodoma ili kujenga hospitali nyingine ya rufaa ya Mkoa ili hospitali ya rufaa ya mkoa ibaki kutoa huduma za kibingwa na kuweza kupunguza mrundikano wa wagonjwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »