WAZIRI JAFO ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI WA MWISHO WA MWEZI SOKO LA BONANZA JIJINI DODOMA

WAZIRI JAFO ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI WA MWISHO WA MWEZI SOKO LA BONANZA JIJINI DODOMA

Na Barnabas Kisengi, Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo Julai 30,2022 ameshiriki katika zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi katika Soko la Bonanza Jijini Dodoma. Akiwa sokoni hapo amezungumza na wafanyabiashara na kutoa rai kwao kudumisha kwa vitendo kampeni ya usafi na mazingira kwa ujumla.“Ndugu

Na Barnabas Kisengi, Dodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo Julai 30,2022 ameshiriki katika zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi katika Soko la Bonanza Jijini Dodoma.


Akiwa sokoni hapo amezungumza na wafanyabiashara na kutoa rai kwao kudumisha kwa vitendo kampeni ya usafi na mazingira kwa ujumla.
“Ndugu zangu agenda ya mazingira ni endelevu sote yatupasa kuitekeleza kwa vitendo na uwe ni utamaduni wetu sote kuwa na tabia ya kufanya usafi katika maeneo yetu”  alisisitiza Dkt Jafo.


Waziri Dkt Jafo amewapongeza wafanyabiashara soko la Bonanza, Waandishi wa habari na mabalozi wa mazingira na wananchi kwa ujumla kwa kujitokeza kushiriki kufanya usafi wa mazingira.


Amemwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ndani ya kipindi cha siku 14 kuhakikisha anafanya ukarabati wa mfumo wa maji taka katika soko hilo la Bonanza ili kuondoa adha inayowakumba wafanyabiashara kwa sasa.
“Ukarabati huu wa Mfumo wa maji taka katika eneo hili ufanyike mara moja, Mkurugenzi wa DUWASA asimamie kwa karibu utekelezaji wake ili wafanya biashara katika sako hili waweza kuondokana na adha hii wanayoipata sokoni hapa” Alisisitiza Dkt. Jafo.


Waziri Jafo amesema kuwa Serikali inatarajia kuzindua Kampeni ya usafi wa mazingira itakayofahamika kama ‘My Dustbin’ kwenye mitaa ya mbalimbali nchi nzima.


Aidha Waziri Dkt Jafo amesema kampeni hiyo itasaidia kuweka mitaa katika hali ya usafi kwa kuwa kila mwananchi anatakiwa kutupa taka kwenye mapipa yaliyoyopo kwenye mitaa badala ya kutupa ovyo.


Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu wa Jiji la Dodoma Bw. Dickson Kimaro amesema wamekuwa wakihamasisha wananchi kushiriki usafi wa mazingira ili kuweka jiji  la Dodoma katika hali ya usafi  Kimaro alilisitiza uwajibikaji wa kila mwananchi katika kuhakikisha usafi unafanyika Mita tano kuzunguka maeneo ya Makazi  na Biashara. 


Kimaro Amesema katika soko hilo wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakijitokeza kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira sokoni hapo hivyo kuliweka jiji katika hali ya usafi.


Baada ya zoezi la Usafi katika soko hilo waziri Dkt Jafo alikutana na mabalozi wa Mazingira na waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Kwa chakula cha pamoja na wanahabari.
“Napenda kuwaambia Waandishi wa Mkoa wa Dodoma ishini kwa upendo mpenda sana katika kazi na nje ya kazi najua kila vyombo vyenu vinakanuni na maadili yake ila hakikisheni nje ya vyombo vyenu mnavyofanyia kazi mnakuwa na upendo wa kupendana hakika mtakuwa na umoja nzuri sana maana kama hampendani hata mwenyezi mungu hapendi kubwa nawachia nieishini kwa upendo na umoja”Amesisitiza Dkt Jafo.


Mussa Yusuph ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Center Press Clab (C.P.C) awali akimkaribisha Waziri Dkt Sellema  Jaffo amesema tukio la mabalozi wa Mazingira na Waandishi wa habari kufanya Usafi katika soko ni jambo la kupelekea licha ya kutumia kalamu zetu bado tumekuwa na chachu ya kusaidiana na jamii Katika kuelimisha juu ya usafi waemazingira na kujitoa kusaidiana na Wananchi katika kufanya usafi kama uliofanyaka leo katika soko.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »