WAKULIMA 15, 000 WANUFAIKA NA ELIMU YA KILIMO TOKA TAASISI YA DCT MKOANI DODOMA

WAKULIMA 15, 000 WANUFAIKA NA ELIMU YA KILIMO TOKA TAASISI YA DCT MKOANI DODOMA

Ña Barnabas Kisengi-Dodoma Mradi wa kilimo hifadhi unaotekelezwa na Taasisi ya Huduma za maendeleo ya Dayosisi ya Central Tanganyika DCT umewanufaisha Wakulima takribani 15,000 wa Wilaya za Dodoma Mjini, Bahi na Wilaya ya Chamwino zilizopo Mkoani Dodoma baada ya kuwapa mafunzo wakulima  kuhusu umuhimu wa Kilimo hifadhi. Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Lister Nyang’anyi  amesema hayo 

Ña Barnabas Kisengi-Dodoma


Mradi wa kilimo hifadhi unaotekelezwa na Taasisi ya Huduma za maendeleo ya Dayosisi ya Central Tanganyika DCT umewanufaisha Wakulima takribani 15,000 wa Wilaya za Dodoma Mjini, Bahi na Wilaya ya Chamwino zilizopo Mkoani Dodoma baada ya kuwapa mafunzo wakulima  kuhusu umuhimu wa Kilimo hifadhi.


Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Lister Nyang’anyi  amesema hayo  Jijini Dodoma wakati akizungumza na J five Blog katika mahojiano maalum kuhusiana na Mradi wa kilimo hifadhi.


Nyang’anyi amesema  kuwa lengo la Mradi wa Kilimo hifadhi ni kuwasaidia Wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuwa na uhakika wa Chakula  kwa ngazi ya Kaya kutokana na Mkoa wa Dodoma kuwa na ukame.


Aidha Nyang”anyi amesema Wamekuwa wanafanya uhamasiahaji kwa Wakulima wa Wilaya tatu za Bahi,Wilaya ya Dodoma Mjini na Wilaya ya Chamwino  kwa kuwaweka katika makundi na kuwapa Elimu hiyo ya kilimo hifadhi.
“Mafunzo ya Kilimo hifadhi ni pamoja na kanuni ya utifuaji uliopunguzwa,kifunika udongo na mchanganyiko wa mazao na hivyo  kumsadia Mkulima kuvuna Maji wakati wa mvua na kuyatunza ili  kusaidia mimea kustawi wakati wa ukame,”Amesema Nyang’anyi


Pamoja na mambo mengine amebainisha kuwa wanatekeleza Mradi huo kwakushirikiana na Halimashauri ya Jiji la Dodoma  ambapo kwa Mwaka huu walipewa eneo kwaajili ya kuonyesha kanuni za kilimo hifadhi kwa wakulima katika Viwanja vya nanenane Nzuguni.


Nyang’anyi Amesema katika eneo la viwanja vya maonyesho ya nane nane mwaka huu 2022 waliweza kutembelewa na jumla ya wakulima 360 wakati wa msimu wa maonyesho ya wakulima nanenane na kutoa elimu ambapo ameahidi kushiriki msimu ujao wa maonyesho hayo ili kuwafikia watu wengi zaidi ili nao wanufaike na Elimu hiyo.


Katika hatua nyingine Nyang’anyi ameeleza Changamoto zilizopo ni ukame ambao huwaathiri Wakulima wengi,Mifugo kuchunga maeneo ya mashamba ikiwemo  kuchoma moto maeneo ya Mashamba.
“Katika kukabiliana na changamoto hizo tumekuwa tunakaa pamoja na Viongozi wa Serikali za Vijiji katika kuweka mkazo juu ya matumizi ya Sheria za mazingira ili kudhibiti vitendo vya uchomaji moto wa Mashamba na  kudhibiti Wanyama waharibifu wa mazao,”Amesisitiza Nyang’anyi
Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wakulima kuzingatia  kanuni za kilimo hifadhi,kutumia Mbegu bora wanazoelekezwa na wataalamu wa Kilimo hasa kwa  Dodoma kupanda  mikundekunde,Choroko,Mbaazi Fiwi na Alizeti ikiwemo  matumizi ya mtama mweupe na uwele.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »