WAKIRISTO KOTE NCHINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

WAKIRISTO KOTE NCHINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA  BIDII

Na Barnabas Kisengi-Mpwapwa Dodoma Wakristo wote hapa nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kuchangi pato la Taifa  na kutatua changamoto zilizo katika maeneo yao.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu GEORGE SIMBACHAWENE amesema hayo  wakati akizunguma katika sherehe ya kumweka wafu Askofu wa  tatu wa Kanisa  la

Na Barnabas Kisengi-Mpwapwa Dodoma


Wakristo wote hapa nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kuchangi pato la Taifa  na kutatua changamoto zilizo katika maeneo yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu GEORGE SIMBACHAWENE amesema hayo  wakati akizunguma katika sherehe ya kumweka wafu Askofu wa  tatu wa Kanisa  la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. GEORGE CHITETO iliyofanyika Jijini Dodoma baada ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Askofu Donald Mtetemela kumaliza muda wake.


Waziri SIMBACCHAWENE amesema chanamoto nyngi za kiuchumi katika jamii zitatauliwa endapo wananchi watajituma kufanya kazi na kuwa wabunifu   kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama ambavyo maandiko matakatifu yanaagiza watu kufanya kazi.
“Lazima wakristo wa sasa tufanye kazi lazima tutatue changamoto kwenye maeneo yetu maana imeandikwa katika biblia asiyefanya kazi na asile kwa hiyo kufanya kazi ndio uhai wetu na heshima yako na ukizalisha utaweza kuendesha maisha yako binfasi, utashiriki katika kazi ya Mungu na Taifa zima” amesisitiza Waziri Simbachawene.


Aidha Waziri SIMBACHAWENE amesema kwamba serikalii itaendelea kushirikiana na taasisi za dini kwani zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo kusimamia maadili na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya watu wasiyo na hofu ya Mungu.
“Licha ya mchango mkubwa wa kanisa hili kwa serikali lakini kumekuwa na mmomonyoko wa maadili, magonjwa na majanga mbalimbali hivyo ni muhimu kushirikiana na serikali ili kuokoa vijana na watoto wetu na matumaini yetu viongozi wa dini mkiendelea kusimama  imara  na kutoa huduma ya kiroho tutatatua changamoto hii” amesisitiza Waziri Simbachawene


Waziri SIMBACHAWENE alibainisha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na RAIS SAMIA SULUH HASSAN imeendelea  kuchukua hatua za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa , ufisadi, utovu wa nidhamu kwa watumishi wa umma pamoja na jamii kwa ujumla.
 Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mhashamu Dr. MAIMBO MNDOLWA ameipongeza serikali kwa kuwa mstari wa mbele kuziunga mkono taasisi za dini  katika nyanja zote huku akimtaka Askofu CHITETO kufanya kazi kwa kumtegemea Mungu hatimaye kufikia malengo ya kanisa yaliyowekwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ROSEMARY SENYAMULE  ametoa  wito kwa wakazi wa mkoa Dodoma kutumia fursa ya serikali  kushusha bei ya  mbolea kwa kujikita katika kilimo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »