WAZIRI UMMY AELEZA CHANZO CHA MFUKO WA BIMA YA AFYA KUELEMEWA

WAZIRI UMMY AELEZA CHANZO CHA MFUKO WA BIMA YA AFYA KUELEMEWA

Ña Barnabas Kisengi-Dodoma Wizara ya Afya imeeleza chanzo ya kuelemewa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwa kuongezeka kwa idadi kubwa ya wananchi wenye magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo gharama zake ni kubwa. Imetaja sababu nyingine inayohatarisha uhai na uendelevu wa Mfuko huo kuwa ni vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu hali ya mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Leo 1 Septemba, 2022 Jijini Dodoma.

Ña Barnabas Kisengi-Dodoma


Wizara ya Afya imeeleza chanzo ya kuelemewa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwa kuongezeka kwa idadi kubwa ya wananchi wenye magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo gharama zake ni kubwa.


Imetaja sababu nyingine inayohatarisha uhai na uendelevu wa Mfuko huo kuwa ni vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma na wanachama wa Mfuko, ambapo amesema vitendo hivyo vinalenga kujipatia manufaa kinyume na utaratibu. 


 Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu hali ya mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambapo hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa sintofahamu hivi karibuni kuhusu mfuko huo.

Waziri Ummy amesema kuhusu kulegalega kwa mfuko huo kutokana na wagonjwa wengi kukata bima wakati wakiwa tayari wameshazidiea.
Waziri Ummy amesema kuwa mnamo Agosti 29 mwaka huu wakati akifungua Mkutano wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu jijini Dar es Salaam aliweka msisitizo wa kuweka nguvu na jitihada katika kuzuia magonjwa badala ya kusubiri kutibu. 
“Katika mukutano huo nilitoa angalizo kuwa hivi sasa nchini kwetu tunashudia ongezeko kubwa la magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo matibabu yake ni gharama kubwa na hivyo kama tutachelewa kuchukua hatua stahiki katika kudhibiti magonjwa hayo, basi kuna hatari pia kwa Mfuko wetu wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuelemewa na gharama za matibabu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanufaika wenye magonjwa yasiyoambukizwa na gharama zake hali inayoweza kuathiri uhai na uendelevu wa Mfuko,”Alisisitiza Waziri Ummy
Waziri Ummy amesema kuwa kulingana na takwimu zilizopo gharama za magonjwa yasiyo ya kuambukizwa zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 35.65 mwaka wa fedha 2016/17 hadi shilingi bilioni 99.09 mwaka fedha 2021/22.


Aidha amesema kuwa gharama za kuhudumia wagonjwa wa saratani wanaopata tiba za mionzi na chemotherapia (chemotherapy services), kupitia Mfuko ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 9 mwaka 2015/16 hadi kufikia shilingi bilioni 22.5 mwaka 2021/22.


Waziri Ummy amesema kwa upande wa huduma za matibabu ya figo kwa wanachama wanaopata huduma ya kuchuja damu (hemodialysis services), gharama ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 9.5 mwaka fedha 2015/16 kufikia shilingi bilioni 35.44 mwaka fedha 2021/22, Pia idadi ya wagonjwa hawa wa figo imeongezeka kutoka 280 mwaka 2014/15 hadi kufikia 2,099 mwaka 2021/22.


Aidha Waziri Ummy amesema gharama za matibabu ya moyo kwa wanachama wa Mfuko wanaopata matibabu ya upasuaji wa moyo (minimal and invasive cardiac procedures), ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 0.5 mwaka 2015/16 hadi kufikia shilingi bilioni 4.33 mwaka 2021/22. 


Huku Gharama za vipimo vya CT scan na MRI ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 5.43 mwaka 2015/16 hadi kufikia shilingi bilioni 10.87 mwaka 2021/22.
“Kwa muelekeo wa takwimu hizi, ni wazi kuwa kama hatutachukua hatua madhubuti kama nchi, kuna uwezekano wa Mfuko kwa siku za mbeleni kushindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria”Alisisitiza Waziri Ummy.


“Hatua hizo zinaanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwa kubadili mtindo wa maisha kwa kuzingatia aina za vyakula tunavyokula, kuepuka uvutaji wa sigara na kufanya mazoezi hata hivyo Serikali kuendelea kubuni mikakati ya kukinga magonjwa haya na pia kupambana nayo kadri yanavyojitokeza”amesema Waziri Ummy.


Akizungumzia vitendo vya udanganyifu vinanavyofanywa na baadhi ya watoa huduma ya Afya,Waziri Ummy amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 jumla ya wataaluma 65 wamefikishwa katika mabaraza yao kutokana na kukiuka taratibu na miongozo ya taaluma za afya. 


Waziri Ummy amesema kuwa  NHIF Sasa iweke mikakati mikubwa ya kuimarisha na kupambana na vitendo vya udanganyifu pamoja na kuimarisha matumizi ya Mifumo ya TEHAMA katika maeneo yake.


Aidha Waziri Ummy amesema Pamoja na hayo alitaja changamoto nyingine iliyopo ni uwepo wa kundi kubwa la wananchi wanaojiunga na NHIF kwa hiari ambao, takribani asilimia 99 ni wagonjwa. 
“Hatua hii imetokana na kutokuwepo kwa Sheria ya ulazima kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya,kama mnavyokumbuka (NHIF)ulianzishwa mwaka 2001 ukiwa umelenga kuwahudumia watumishi wa umma pekee”amesema Waziri Ummy.


Waziri Ummy amesema ni wazi kuwa hali ya ustahimilivu na uendelevu wa Mfuko ipo mashakani endapo hatua stahiki hazitachukuliwa. 


Waziri Ummy ametaja hatua hizo kuwa ni kuimarisha afua za kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza  katika hatua za awali ikiwemo kuyatambua mapema kabla ya kuwa na athari kubwa,kuongeza idadi ya wanachama,kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya,kudhibiti matumizi ya huduma yasiyo na tija,kupunguza gharama za matibabu nchini na kuwa na Mfumo endelevu wa kuhakikisha Mfuko unakuwa na fedha wakati wote kutoka katika vyanzo vyake vya mapato.
“Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ambayo itaweka mazingira kwa kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuwezesha dhana ya kuchangiana gharama za matibabu na hivyo kuwaepusha wananchi katika hatari ya janga la umaskini pindi wakiwa wagonjwa au wanapougua,”Amesisitiza Waziri Ummy.


Aidha Waziri Ummy amewatoa hofu wanachama  wa NHIF na wananchi kwa ujumla kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuuimarisha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuwa endelevu na kuwanufaisha wananchi walio wengi zaidi. 
“Hatutakubali kuona Mfuko huu unatetereka kwa sababu Changamoto zilizoko tunazifahamu na mikakati ya kuzishughulikia imeanza kutekelezwa,”amesema Waziri Ummy
.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »