KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YAIPONGEZA WIZARA YA ELIMU USIMAMIZI WA WELEDI WATUMISHI KUHAMIA DODOMA

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YAIPONGEZA WIZARA YA ELIMU USIMAMIZI WA WELEDI WATUMISHI KUHAMIA DODOMA

Na Mathias Canal, WEST-Dodoma Kamati ya Huduma na Maendeleo ya jamii imempongeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda kwa kusimamia kwa weledi na ufanisi uratibu wa zoezi la watumishi kuhamia Jijini Dodoma kuitikia maelezo ya serikali. Kauli hiyo ya pongezi imetolewa leo tarehe 8 Septemba 2022 na Mwenyekiti wa kamati hiyo

Na Mathias Canal, WEST-Dodoma

Kamati ya Huduma na Maendeleo ya jamii imempongeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda kwa kusimamia kwa weledi na ufanisi uratibu wa zoezi la watumishi kuhamia Jijini Dodoma kuitikia maelezo ya serikali.

Kauli hiyo ya pongezi imetolewa leo tarehe 8 Septemba 2022 na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Stanslaus Nyongo (Mb) wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) Jijini Dodoma.

Mwenyekiti Nyongo amesema kuwa Wizara hiyo imetii kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuhamia Dodoma ambayo ni maelezo muhimu yaliyotolewa na serikali.

Mhe Nyongo amesema kuwa kujengwa kwa ofisi na kuhamia Jijini Dodoma kutarahisisha wananchi kupata huduma kwa urahisi na ukaribu kwani huduma hiyo ni muhimu kwa Usalama wao na usalama wa Taifa kwa ujumla.

“Sisi kama kamati tumeridhika kwa kuja na kuona na tunaahidi tutakuja tena kujionea kazi zinazofanywa pindi jengo litakapoanza kutumika” Amekaririwa Mhe Nyongo

Mwenyekiti huyo ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha kuwa inawatangazia wananchi kwa kila hali ili waweze kujua kuwa huduma zimerahisishwa na tayari zinapatikana makao makuu ya nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema kuwa ziara hiyo ya kamati ya Bunge kuangalia ujenzi wa ofisi za kitaifa za Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) imefikia hatua nzuri za ujenzi na hiyo ni sehemu muhimu katika utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhamia Jijini Dodoma.

Waziri Mkenda amesema kuwa utekelezaji huo wa maelekezo ya serikali unaenda sambamba na ujenzi wa majengo ya Taasisi za Wizara ili wafanyakazi wanapohamia Dodoma wawe na sehemu ya kufanyia kazi na Taasisi isikodi sehemu ya kuafanyia kazi.

Kadhalika amempongeza Mtendaji Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomoki Prof Lazaro kwa utekelezaji mzuri wa ujenzi wa Ofisi Jijini Dodoma ambao umefikia asilimia 85

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »