ALHAJ DK.MWINYI SALA IJUMAA MASJID LOOTAH KIEMBE SAMAKI

ALHAJ DK.MWINYI SALA IJUMAA MASJID LOOTAH KIEMBE SAMAKI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani iliopo ili  Serikali iweze kufikia malengo ya kuwaletea maendeleo. Alhaj Dk. Mwinyi amesema hayo katika salamu alizotoa kwa waumin walioshiriki Ibada ya sala ya ijumaa iliofanyika Masjid Lutta, Kiembesamaki Mkoa Mjini Magharibi. Amesema hivi sasa nchi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani iliopo ili  Serikali iweze kufikia malengo ya kuwaletea maendeleo.

Alhaj Dk. Mwinyi amesema hayo katika salamu alizotoa kwa waumin walioshiriki Ibada ya sala ya ijumaa iliofanyika Masjid Lutta, Kiembesamaki Mkoa Mjini Magharibi.

Amesema hivi sasa nchi ina amani ya kutosha, hivyo ni wajibu wa wananchi kuendeleea kudumisha hali hiyo, ili kutoa fursa kwa Serikali kutekelza malengo yake ya kuwaletea maendeleo.

Aidha, aliwataka wananchi popote pale walipo kufanya juhudi  kutimiza wajibu wao ili  waweze kupata mafanikio.

Nae, Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwaomba waumini kumuombea Dua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Mwinyi ili amfanyie wepesi katika kutekeleza malengo yake ya kuiletea nchi maendeleo.

Mapema, Khatibu katika sala hiyo ya Ijumaa Sheikh Said Khalfan Said aliwataka waumini kurudi kwa Mwenyezi Mungu na kutekeleza maamrisho yake pamoja na kumshukuru kwa neema ziliopo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »