SERIKALI KUWAREJESHA WATOTO WA MITAANI KUUNGANA NA FAMILIA ZAO

SERIKALI KUWAREJESHA WATOTO WA MITAANI KUUNGANA NA FAMILIA ZAO

 Yawataka Wazazi na Walezi Kuwasikiliza Watoto Ndoto Zao Familia Ziepuke Migogoro Kupunguza Wimbi la Watoto wa Mitaani Na Mwandishi Wetu, WMJJWMM, Dar Es Salaam Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza utaratibu wa kuwarejesha watoto wa mitaani kuungana na familia zao ili kupunguza wimbi la ongezeko la watoto hao kwenye maeneo ya mijini kwa

 Yawataka Wazazi na Walezi Kuwasikiliza Watoto Ndoto Zao

Familia Ziepuke Migogoro Kupunguza Wimbi la Watoto wa Mitaani

Na Mwandishi Wetu, WMJJWMM, Dar Es Salaam

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza utaratibu wa kuwarejesha watoto wa mitaani kuungana na familia zao ili kupunguza wimbi la ongezeko la watoto hao kwenye maeneo ya mijini kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanapata malezi stahiki .

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya maeneo ya Ubungo mkoani Dar es Salaam ambapo alikutana na kikundi cha watoto wa mitaani wanaoishi na kuomba omba maeneo hayo ya barabara na kulazimika kulala pembezoni mwa barabara hiyo ikiwemo juu ya miti kwa kufunga viota na kulala juu mithili ya ndege

Akizungumza na watoto hao wenye umri kati ya miaka 12 hadi 17, Waziri Dkt. Gwajima alibaini kuwa watoto hao wamechoka kuishi maisha ya kuomba omba na wako tayari kurejea mikoa waliyotoka ili kuungana na familia zao kwa kuwa kupitia maisha hayo wamekutana na changamoto mbali mbali ikiwemo kutumiwa na baadhi ya wananchi kuwafanyia biashara na kuwapa ujira mdogo; kujiunga na makundi ya vijana wavuta bangi na watumiaji wa madawa ya kulevya; kushiriki vitendo vya wizi, ulawiti, ubakaji; na kupata magonjwa mbali mbali ambayo yanahatarisha afya na kupoteza ndoto za maisha yao ya baadae

Amewataka watoto wote wa mitaani waliopo maeneo mbali mbali nchi nzima kutoa ushirikiano kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ili Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo wamiliki wa vyombo vya usafiri na Jeshi la Polisi kuwasafirisha watoto hao ili waungane na familia zao.

Waziri Dkt. Gwajima amewataka wazazi kusikiliza ndoto za watoto wao na kubaini wanachohitaji ili waweze kusoma na kufikia malengo yao badala ya kuwapotezea malengo waliyonayo kwa ajili ya maisha yao ya baadae

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula aliwachukua watoto hao zaidi ya ishirini na kupelekwa nyumba ya makao maalum ili waweze kupatiwa ushauri nasaha, kuwaandaa kisaikolojia, kupatiwa huduma za afya na kuandaliwa kwa ajili ya kusafirishwa kurejea kwa wazazi ili kuungana na familia

Watoto hao walisema kuwa baadhi ya watoto wanakimbia familia zao na kujiunga na maisha ya kuwa na watoto wa mitaani sio kwa sababu wazazi hawana uwezo au wamefariki bali ni kwa sababu ya migogoro iliyopo kwenye familia mathalani wazazi kutengana, migoro ya urithi ambayo inasababisha watoto wakimbilie mitaani ili kuepuka kuishi na mzazi wa kambo au kwa ndugu badala ya kuishi na wazazi wake

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »