MWONGOZO WA KITAIFA WA UANZISHAJI MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI WAZINDULIWA

MWONGOZO WA KITAIFA WA UANZISHAJI MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI WAZINDULIWA

Na WMJJWM Pwani Serikali imezindua Mwongozo wa Kitaifa wa Uanzishaji na Uendeshaji Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wenye lengo la kuleta ufanisi wa utekelezaji wa majukwaa haya ikiwa ni pamoja na kuyafanya yajulikane ngazi zote hapa nchini. Akizungumza katika Uzinduzi wa Mwongozo huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia

Na WMJJWM Pwani


Serikali imezindua Mwongozo wa Kitaifa wa Uanzishaji na Uendeshaji Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wenye lengo la kuleta ufanisi wa utekelezaji wa majukwaa haya ikiwa ni pamoja na kuyafanya yajulikane ngazi zote hapa nchini.


Akizungumza katika Uzinduzi wa Mwongozo huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima ameitaka jamii kuelimisha Wanawake waone umuhimu wa kujiunga na majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kuanzia ngazi ya kijiji/Mtaa, Kata, Wilaya hadi Taifa, ili yawawezeshe kupata sehemu ya kujadili mambo yao kuhusu ujasiriamali na biashara kwa ujumla.
Pia amezitaka Halmashauri za Wilaya/Manispaa na Majiji ziendelee kutenga Fedha za ndani ili kuwawezesha Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kukopa na hatimaye kuweza kujiendeleza kiuchumi.


Ametoa rai kwa Wanufaika wa Mikopo ya Asilimia 10 na mikopo ya Maendeleo ya Wanawake (WDF) inayotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii wahakikishe wanarejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iwanufaishe wengine kupata mikopo mapema. 
Vilevile Waziri Dkt. Gwajima ameitaka jamii kutoa fursa sawa kwa Wanawake na wanaume kushiriki nafasi za uongozi na maamuzi katika ngazi ya jamii na kuwa sehemu ya maamuzi kwa ustawi wa jamii na Taifa letu.  
“Wanawake na wanaume tuzidi kuungana kupinga ukatili wa kijinsia na kwa watoto kwa kusimamia kurithisha misingi ya maadili mema kwa vizazi vyetu kwani ukatili ni adui wa maendeleo ya kiuchumi.” alisema Waziri Dkt Gwajima  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Sarah Msafiri amesema kuwa, kupitia Mwongozo huo Mkoa wa Pwani umeanzisha Kampuni ya Go Mama PLC inayofanya shughuli zake ndani ya Mkoa.


Akieleza kuhusu Mwongozo huo Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula amesema Wizara iliona umuhimu wa kuwa na Mwongozo wa Uanzishaji na Uendeshaji Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ili kuwa na ufanisi katika ushiriki wao hususani kwenye shughuli za maendeleo zitakazosaidia kuwakwamua kiuchumi.


Akitoa salamu za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Zanzibar Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mariam amesema Wizara itasimamia utekelezwaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Uanzishaji na Uendeshaji Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ili kuwawezesha Wanawake hasa wajasirimali kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli zao mbalimbali.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara (TWCC) Mwajuma Hamza amesema Chama hicho kimefarijika kuona kuwa Serikali imejipanga ili kuhakikisha inawezesha Wanawake hasa katika kuwakwamua kiuchumi kwa kuweka Miongozo itakayo saidia kuratibu uanzishwaji na Uendeshaji wa Majukwaa hao.
Akizungumza katika uzinduzi wa Mwongozo huo Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bein’g Issa amesema Baraza lao limeweka mikakati mbalimbali yani kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwa kushirikiana na Wizara walitarubu uanzishwaji wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kwa ngazi za Vijiji/ Mitaa, Kata, Wilaya na Mkoa.


Ameongeza kuwa uanzishwaji wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi umesaidia kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake wajasirimali jumala ya Majukwaa 26 yameamzishwa katika Mikoa ya Tanzania Bara, Majukwaa 151 katika Halmashauri, Majukwaa 1354 ngazi ya Kata na Majukwaa 1859 katika ngazi ya vijijini/ Mitaa.
“Katika haya yote Mikoa mingi imefanya ubunifu ikiwemo kuanzishwa kwa makampuni, vikundi vya wajasirimali ambapo imesaidia kuwawezesha kiuchumi Wanawake hasa wajasirimali” alisema Bi. Bein’g.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake Mkoa wa Pwani Mariam Ulega ameishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha inaweka mifumo mizuri ya kuwawezesha Wanawake hasa wajasirimali kupata fursa za kuanzisha biashara na kupata masoko ya bidhaa zao kwa ustawi na maendeleo ya familia na taifa

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »