UWT KATA YA KILIMANI YAPATA UONGOZI MPYA

UWT KATA YA KILIMANI YAPATA UONGOZI MPYA

Na Barnabas Kisengi Dodoma Chama cha Mapinduzi kata ya KILIMANI Jijini Dodoma kimekamilisha kufanya uchaguzi wa jumuiya ya wanawake UWT kata ya KILIMANI na kuwapata viongozi wa kata hiyo baada ya uchaguzi huo kuhairishwa mara kwa mara. Uchaguzi huo wa jumuiya ya wanawake UWT kata ya KILIMANI umekamilika kwa kumpata Mwenyekiti na katibu wa UWT

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Chama cha Mapinduzi kata ya KILIMANI Jijini Dodoma kimekamilisha kufanya uchaguzi wa jumuiya ya wanawake UWT kata ya KILIMANI na kuwapata viongozi wa kata hiyo baada ya uchaguzi huo kuhairishwa mara kwa mara.


Uchaguzi huo wa jumuiya ya wanawake UWT kata ya KILIMANI umekamilika kwa kumpata Mwenyekiti na katibu wa UWT na wajumbe wa baraza la jumuiya ya wanawake UWT kata ya KILIMANI.


Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni  Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya jumuiya ya Umoja wa wazazi wilaya Bi HADIJA HAMSINI amesema chama cha Mapinduzi kupitia jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT kimetumia demokrasia kwa Wanawake wote waliochukua fomu na kujitokeza kwa wale walio kuwa na sifa wameweza kuingia kwenye king’ang’aniro cha uchaguzi huo.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo wa jumuiya ya wanawake UWT kata ya KILIMANI Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya jumuiya ya Umoja wa wazazi wilaya Bi HADIJA HAMSINI amesema nafasi zilizokuwa zikiwaniwa ni nafasi ya wajumbe wa baraza UWT kata nafasi zilikuwa Tano na waliogombania walikuwa kumi na Tano.


Bi HADIJA HAMSINI amewataja washindi waliochaguliwa kuwa wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT kata ni Faustina Bendera, Ester Stanley, Nasra Mjili, Masele Issa na Happiness Ndilo.


Aidha msimamizi wa uchaguzi huo wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT kata ya KILIMANI Bi HADIJA HAMSINI amesema kwa nafasi nyingine ilikuwa nafasi ya katibu UWT kata ya KILIMANI wagombea walikuwa 3 kura zilizopigwa zilikuwa 14  na matokeo yalikuwa Victoria Wanyange kura 0, Emmalenciana komba kura 3,na Vannosa Matawa kura 11 hivyo kwa mamlaka niliyonayo namtangaza Vannosa Matawa kuwa katibu wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT kata ya KILIMANI.


Bi HADIJA HAMSINI akaanza nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya ya wanawake UWT kata ya KILIMANI wagombea nafasi hiyo walikuwa 3 kura zilizopigwa na wajumbe wa mkutano Mkuu wa UWT kata zilikuwa 16 ambapo Raha Mpera alipata kura 0, Irene Chilewa amepata kura 4 na Melina Lumolwa amepata kura 12 kwa mamlaka niliyonayo ninamtangaza Melina Lumolwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa jumuiya ya wanawake UWT kata ya KILIMANI.


Chama cha Mapinduzi kata ya KILIMANI kimemaliza chaguzi zake Zote kuanzia mashina, matawi na kata na Sasa chaguzi hizi zinaendelea kwa ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa.


Ikumbukwe chama cha mapinduzi kila baada ya miaka 5 kimekuwa na destuli ya kufanya chaguzi ndani ya Chama ili kuweza kupata viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya shina, Tawi, kata, wilaya, Mkoa na Taifa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »