Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amewataka Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za MajiSafi na Usafi wa Mazingira nchini kushughulikia changamoto za wananchi zinazohusiana na upatikanaji wa huduma bora ya Maji. Ameyasema haya wakati akifunga kikao kazi cha Wakurugenzi Watendaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kilichofanyika mkoani Morogoro. Aidha Waziri Aweso ameeleza kuwa Wakurugenzi wa
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amewataka Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za MajiSafi na Usafi wa Mazingira nchini kushughulikia changamoto za wananchi zinazohusiana na upatikanaji wa huduma bora ya Maji.
Ameyasema haya wakati akifunga kikao kazi cha Wakurugenzi Watendaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kilichofanyika mkoani Morogoro.
Aidha Waziri Aweso ameeleza kuwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji wawe karibu na jamii na zaidi wawe na Utamaduni mzuri wa kupokea taarifa na kuzifanyia kazi pamoja na kutoa taarifa kwa wananchi pale inapobidi ili kutengeneza daraja zuri la mawasiliano kati yao na wananchi.
Pamoja na haya amezitaka mamlaka ambazo zinaendelea na Utekelezaji wa Miradi zihakikishe zinakamilisha miradi hii kwa haraka kwani baada ya Bunge ataanza ziara rasmi kupita maeneo yote nchini kufatilia utekelezaji wa Miradi ya Maj.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *